Home Habari za michezo UNAAMBIWA HUYO AYOUB WA SIMBA BADO HAJAANZA BALAA LAKE

UNAAMBIWA HUYO AYOUB WA SIMBA BADO HAJAANZA BALAA LAKE

Tetesi za Usajili Simba

Kocha wa makipa wa Simba, Dani Cadena amesema kiwango kinachoonyeshwa na kipa Ayoub Lakred ni asilimia ndogo na mashabiki wa kikosi hicho watarajie mambo makubwa kwake msimu huu licha ya kuanza kwa kusuasua kikosini.

Ayoub juzi kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Wydad AC ya Morocco alionyesha kiwango bora ikiwa ni mwendelezo wa moto aliouonyesha kwenye michuano ya CAF na kuiwezesha timu hiyo kushinda mabao 2-0 ikapanda kutoka nafasi ya nne ya Kundi B hadi ya pili ikiwa na pointi tano.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Cadena alisema kipa huyo alianza taratibu kutokana na kutozoea mazingira ya hapa nchini na hata wachezaji wenzake kiujumla ingawa kwa kipindi kifupi ameanza kuzoea ndio maana anafanya vizuri.

“Kila mmoja ni lazima atambue Lakred ni kipa mzuri lakini kwa bahati mbaya kwake alianza taratibu na ukiangalia mahitaji ya timu kiujumla yalikuwa makubwa hivyo kumpelekea presha ambayo kwa kiasi kikubwa ilichangia kuanza vibaya,” alisema.

Cadena aliongeza uimara na uvumilivu wake kikosini ndio unamfanya kufanya vizuri huku akiwataka mashabiki watarajie mambo makubwa kutoka kwake.

Lakred aliyejiunga na kikosi hicho msimu huu akitokea FAR Rabat ya Morocco alianza vibaya jambo lililosababisha afanya makosa mara kwa mara ingawa sasa amekuwa tegemeo baada ya Aishi Manula kupata majeraha. Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, Lakred alipata wastani wa asilimia 7.4 wa kiwango bora kwa mujibu wa mtandao wa Fotmob akipitwa na Leandre Onana aliyepata 8.9.

Katika ligi hiyo, Lakred yupo nafasi ya tatu kwa makipa waliookoa michomo mingi golini ambapo amefanya hivyo kwa asilimia 85.7 akipitwa na Hugo Marques wa Petro de Luanda mwenye 100 na Alioune Badara Faty wa TP Mazembe mwenye 90.9. Simba zaidi makala ya kipa huyu ukurasa wa 7

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUONYESHA KIWANGO KIKUBWA...SAIDO MBIONI KUIKIMBIA YANGA...ISHU YA MKATABA YATAJWA...