Home Habari za michezo KAMA YANGA INATAKA USHINDI LEO BASI JAMBO HILI LAZIMA WALIACHE

KAMA YANGA INATAKA USHINDI LEO BASI JAMBO HILI LAZIMA WALIACHE

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga inashuka dimbani hii leo kuikabili Medeama katika ardhi ya ugenini.Yanga inatafuta alama tatu za kwanza ili kufufua matumaini yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii.

Kama Yanga itapoteza hii leo basi itakuwa na mazingira magumu sana ya kusonga mbele kwani itakuwa imesalia na alama moja (1) na watatakiwa kushinda michezo yote mitatu iliyosalia huku wakisubiri miujiza mingine kutendeka.

Kama Yanga itaibuka na ushindi hii leo basi itakuwa imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Mimi ninachoona kama malengo ya Yanga mwanzo yalikuwa ni kufika hatua ya makundi na wametimiza malengo yao, basi wawapunguzie presha wachezaji wao wawape uhuru wa kucheza bila presha kwasababu lengo lao mama wameshalitimiza.

Kama wachezaji watacheza bila presha leo tutegemee kuiona Yanga ikivuna alama tatu muhimu, huu ni mchezo wa saikolojia tu sasa hivi kwa Yanga na mbinu kiasi.

Wakiingia na mbinu nyingi basi inaweza kuwafanya wasipate kile walichokitarajia. Medeama wanacheza kwa kurelax sana kitu ambacho kitakuwa hatari kwa Yanga kama wakikamia show.

Kila la kheri kwa wawakilishi wa nchi hii leo, Tanzania ipo pamoja nanyi.

SOMA NA HII  STAA WA YANGA ACHEKELEA MATOKEO YA SIMBA MBEYA...AWAPONGEZA..AWAOMBEA MATOKEO ZAIDI...