Home Habari za michezo KOMBE LA MAPINDUZI LAMVURUGA GAMONDI

KOMBE LA MAPINDUZI LAMVURUGA GAMONDI

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamond amesema moja ya changamoto wanayokabiliana nayo ni uchovu wa wachezaji kutokana na kuwa na mechi za viporo sambamba na kuwepo kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 inayoanza rasmi Desemba 28 visiwani Zanzibar.

Gamondi ameyasema hayo jijini Dodoma leo Ijumaa, Desemba 22, 2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Tabora United utakaochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

“Wachezaji nao ni binadamu, kuna kuchoka, kuna kuumia ukiachilia mbali tuna viporo hivyo tunalazimika kucheza kkila baada ya siku tatu, jambo ambalo linachosa zaidi wachezaji.” ameongeza Gamondi

Kocha huyo raia wa Argentina amesema wachezaji wapo fiti kuibabili Tabora, licha ya uchovu, huku akitamba kuendelea na aina yake ya uchezaji wa kuwashambulia mfululizo wapinzani.

Yanga ilikuwa inakabiliwa na mechi tatu za viporo, ukiwamo wa kesho na nyingine mbili dhidi ya Kagera Sugar na Mashujaa zilizokuwa zipigwe kati ya Desemba 26 na 29, lakini zimeahirishwa kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi, Yanga ikipangwa kuanza na Bandari Kenya siku ya Desemba 31.

Kamati ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2024 imepanga mchezo huo kupigwa kuanzia saa 2:15 usiku kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar na Kocha Gamondi anaona kama wachezaji hawapati muda wa kupumzika wakati ligi ikisimama kupisha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 itayofanyika mwakani kati ya Januari 13 na Febaru 12 huko Ivory Coast, huku Tanzania ikiwa moja ya nchi shiriki.

SOMA NA HII  ISHU YA PENALTI YA DABI, MWAMUZI FIFA AFUNGUKA NAMNA HII