Home Habari za michezo KUMBE AZIZI KI HANA HAJA NA KIATU LIGI KUU…… MWENYEWE AFUNGUKA HAYA

KUMBE AZIZI KI HANA HAJA NA KIATU LIGI KUU…… MWENYEWE AFUNGUKA HAYA

Habari za Yanga SC

KIUNGO Mshambulijai wa Yanga, Stephane Azizi Ki amesema kuwa licha ya kuwa kinara katika mbio za ufungaji bora wa Ligi Kuu Bara lakini hafikirii kabisa kuwa mfungaji bora na badala yake anafikiria kuisaidia timu hiyo kusonga mbele zaidi.

Azizi Ki kwa sasa diye kinara wa upachikaji mabao ndani ya ligi kuu akiwa ana mabao 10 akifuatiwa na Jean Baleke wa Simba mwenye mabao 8 sawa na Feisal Salum wa Azam FC huku Maxi Nzegeli wa Yanga akiwa na mabao 7.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Azizi Ki alisema kuwa malengo yake yeye binafsi ni kuona anaweza kuisaidia timu yake kupata alama tatu katika kila mchezo ambao upo mbele yao na wala sio kuwaza kuwa mfungaji bora kama ambavyo watu wanasema na wanavyomuambia.

“Nafahamu Wanayanga wengi wanatamani kuona kuwa mimi nakuwa mfungaji bora msimu huu lakini niwaambie tu kuwa kati ya ubingwa wa ligi na mimi kuwa mfungaji bora ipi inapendeza zaidi?

“Mimi binafsi nafurahi kuona naisiadia timu yangu na wala siwazi kabisa suala la kumaliza kuwa mfungaji bora wa ligi hii,” alisema Azizi Ki.

SOMA NA HII  ABDI BANDA YUPO SALAMA HANA CORONA