Home Habari za michezo KWA TAKWIMU HIZI WANANCHI WATATOBOA LEO DHIDI YA MADEAMA

KWA TAKWIMU HIZI WANANCHI WATATOBOA LEO DHIDI YA MADEAMA

Habari za Yanga

Ligi ya Mabingwa Afrika inaendelea kurindima tena leo Desemba 8, 2023 huku Wawakilishi wa NCHI, Young Africans SC wakitupa karata yao ya tatu ya hatua ya makundi.

Medeama vs Yanga SC
Uwanja: Baba Yara
Muda: Saa 1:00 Jioni

Wananchi wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza 3-0 dhidi ya CR Belouizdad, sare ya 1-1 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa pili.

Wananchi wakihitaji ushindi tu ili kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali. Kipigo au sare nyingine vitafifisha matumaini hayo.

MSIMAMO KUNDI D
1. Al Ahly (pointi 4)
2. Medeama (3)
3. CR Belouizdad (3)
4. Yanga SC (1)

MECHI ZINGINE LEO #CAFCL
19:00 || Al Ahly vs CR Belouizdad
22:00 || Etoile Sahel vs Al Hilal Omdurman.

Wananchi watatoboa leo?

SOMA NA HII  BEKI YANGA AKUBALI UWEZO WA MTUPIAJI NAMBA MOJA WA SIMBA