Home Habari za michezo RASMIII….OKRAH AKUNJA MIWILI YANGA….MKWANJA ATAKAOCHUMA NI KUFRU TUPU ….

RASMIII….OKRAH AKUNJA MIWILI YANGA….MKWANJA ATAKAOCHUMA NI KUFRU TUPU ….

Tetesi za Usajili Yanga leo

YAMETIMIA! Winga wa zamani wa Simba, Augustine Okrah sasa ni Mwananchi. Mghana huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga akipewa mkataba wa miaka miwili ili kuitumikia timu hiyo na ataanza kazi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Kiungo mshambuliaji huyo aliichezea Simba msimu wa 2022 na kushindwa kudumu katika timu hiyo kabla ya kuondoka kwenye dirisha kubwa lililopita akiwa na mabao manne na asisti moja, likiwamo bao aliloitungua Yanga kwenye Kariakoo Derby iliyoisha kwa sare ya 1-1 iliyopigwa Oktoba 23, mwaka jana.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga na kwa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo zimethibitisha kuwa, winga huyo tayari amemwaga wino akisaini mkataba wa miaka miwili na atatambulishwa na timu hiyo Zanzibar kabla ya mchezo wa Kombe la Mapinduzi wa Kundi C dhidi ya Jamhuri.

Aidha pia inaelezwa kuwa atalipwa mshahara wa karibu dola 7000 za kimarekani, ambayo ni sawa na zaidi ya milioni 16 kwa pesa za kitanzania, pia Okrah atapewa usafiri, nyumba kali ya kuishi, ambapo mara nyingi wachezaji wote wa kigeni hupewa nyumba maeneo ya Avic Town kigamboni.

“Okrah yupo Tanzania na tayari ameshamalizana na uongozi, kinachosubiriwa ni utambulisho na kuanza kazi ya kuitumikia timu hiyo akianza na michuano ya Mapinduzi,” kilisema chanzo hicho kilichoongeza;

“Usajili wa mchezaji huo umefuata ripoti ya kocha Miguel Gamondi aliyeomba kusajiliwa winga mmoja mwenye kasi na nguvu ili kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji na uongozi ukaona Okrah ndio chaguo sahihi.”

Tangu atue Bechem United ya Ghana, nyota huyo amefunga mabao tisa katika mechi 15 akilingana na Isaac Mintah wa Aduana.

Rafiki wa karibu wa mchezaji huyo ambaye pia hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, Yanga wamefanya uamuzi sahihi kumsajili huku akikiri kuwa mchezaji huyo baada ya kutoka Tanzania na kurudi Ghana alirejea katika ubora wake.

“Okrah ni mchezaji mzuri na Yanga ilivyo sasa ina wachezaji wengi wenye ubora, kama watampa nafasi atafanya kitu kikubwa kama alivyofanya kwenye timu ambayo anaitumikia sasa akiwa ni kinara wa ufungaji baada ya kufunga mabao tisa katika michezo 15 aliyocheza pia anaongoza kwa kutoa pasi za mwisho japo sina uhakika zaidi ana asisti ngapi ila anaongoza,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Nina imani kubwa na mchezaji huyo atakuja kucheza kwa ubora mkubwa, anajua alipokosea msimu uliopita na hawezi kurudia makosa, naamini atakuwa bora zaidi.”

MOLOKO, MUSONDA MTIHANI

Wakati Okrah akitajwa kumalizana na Yanga nyota huyo atahatarisha vibarua vya baadhi ya wachezaji kutokana na kumudu kucheza nafasi hizo huku pia akiwa ni mchezaji ambaye atasaidiana na utatu wa Stephane Aziz Ki, Pacome Zouzou na Maxi Nzengeli kutokana na nafasi hiyo pia kuwa na uwezo nayo.

Okrah anaweza kucheza nafasi tatu uwanjani, wingi ya kulia na kushoto na pia anaweza kucheza kama mashambuliaji namba 10 eneo ambalo limekuwa na wachezaji wanaofanya vizuri kwa sasa wakiongozwa na Aziz Ki aliyetupia mabao 10 hadi sasa.

Katika kucheza kama kiungo wa pembeni ama winga, ni dhahiri anaenda kumpa changamoto Moloko ambaye amekuwa akitumiwa zaidi eneo hilo sambamba na Musonda, hivyo mastaa hao watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanapambania namba zao.

KONKONI, GIFT MH!

Wakati Yanga ikiwa tayari imefanya sajili mbili moja ya mchezaji mzawa Shekhan Ibrahim Khamis kutoka JKU ya Zanzibar na Okrah kutoka Ghana, inasemekana mabingwa hao wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kuachana na mshambuliaji Hafiz Konkoni na beki Gift Fredy kupisha usajili mpya.

Yanga inaendelea kuwinda saini ya mshambuliaji mmoja mgeni baada ya Konkoni kushindwa kufanya kilichotarajiwa kutoka kwake huku Gift akikosa nafasi mbele ya Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job.

Credit- Mwanaspoti

SOMA NA HII  MCHAMBUZI AMPA USHAURI HUU ROBERTINHO LEO DHIDI YA AL AHLY