Home Habari za michezo SIMBA KUWATUMIA KAGERA SUGAR KAMA DARAJA LIGI KUU, UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

SIMBA KUWATUMIA KAGERA SUGAR KAMA DARAJA LIGI KUU, UONGOZI WAFUNGUKA HAYA

Simba SC

Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, amesema wanahitaji ‘ufufuo’ kupitia Kagera Sugar Ijumaa hii katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC.

Ahmed ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Simba Queens dhidi ya JKT Queens katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar na Simba kuibuka na ushindi wa penalti 5-4.

“Tunahitaji ufufuo kupitia Kagera Sugar, tukishamalizana na Kagera tutahamia kwa Wydad AC mchezo ambao hakuna mwanaSimba atabaki nyumbani, wote twendeni Benjamini Mkapa kuhakikisha tunamfanya vibaya Wydad,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  MAJANGA HAFIZ KONKANI AGOMA KUVAA VIATU VYA MAYELE, ISHU IKO HIVI