Home Habari za michezo MTAMBO HUU WA KUFUNGA MAGOLI KUTUA YANGA….KILA KITU KIMEKAMILIKA…

MTAMBO HUU WA KUFUNGA MAGOLI KUTUA YANGA….KILA KITU KIMEKAMILIKA…

Tetesi za usajili Yanga

MSHAMBULIAJI wa Dynamo Dougla ya Cameron, Leonel Ateba  amekamilisha mazungumzo na makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka miwili na uongozi wa Yanga katiika usajili wa dirisha hili dogo la usajili linaloyarajiwa kufungwa Januari 15, 2024.

Taarifa za uhakika kuwa nyota huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo inayokwenda visiwani Zanzibar katika michuano ya kombe la Mapinduzi na kuanza mechi ya kwanza dhidi ya Jamhuri, Desemba 31, mwaka huu.

Mtoa habari huyo amesema tayari mshambuliaji huyo amemalizana na Yanga na kuja kuziba nafasi ya Fiston Mayele ambayo hadi sasa hawajapata mrithi wake na kuamini Ateba anakuja kukata kiu yao.

“Ateba amemalizana na Yanga na muda wowote anatua nchini kuungana na kikosi kwa ajili ya kwenda visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi, atakuwa sehemu ya kikosi,” alisema mtoa habari huyo.

Ameongeza kuwa ujio wa mshambuliaji huyo una wafungulia milango ya kwa kheri nyota wawili, Hafiz Konkoni na Gift Freddy, wakatolewa kwa mkopo kwa sababu wamrshindwa kupata nafasi na kumshawishi kocha Miguel Gamondi kuwapa namba.

Alipotafutwa Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema usajili umeshafanyia (hajataja jina) na wamekamilisha kila kitu na wanatarajia kuonekana katika mchezo wa kwanza wa kombe la Mapinduzi.

“Tumefanya usajili kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi, moja ya sajili zetu tutazioa katika mechi zetu za Mapinduzi tukianza dhidi ya Jamhuri,” alisema Kamwe.

Aliomgeza kuwa kikosi kinaondoka kesho kuelekea visiwani Zanzibar na huku wakitangaza hali ya hatari kwa wapinzani wao kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi na kuendeleza kasi yao ya Ligi Kuu Tanzania.

Yanga wanaondoka na wachezaji wote ambao hawako katika majukumu ya timu zao za Taifa pamoja na wachezaji wapya bao wamesajiliwa kipindi cha dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2024.

SOMA NA HII  WAAMUZI HAWA WAWEKA REKODI MBELE YA RAIS MAGUFULI