Home Habari za michezo SIKU CHACHE BAADA YA KUTANGAZWA… BENCHIKHA KAIBUKA NA HILI KUHUSU USAJILI WA...

SIKU CHACHE BAADA YA KUTANGAZWA… BENCHIKHA KAIBUKA NA HILI KUHUSU USAJILI WA SARR…

Habari za Simba leo

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha sasa ana amani ya moyo mara baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji raia wa Senegal, Babacar Sarr ambaye kwa sasa rasmi ni mali ya Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC tayari wamemtambulisha kiungo huyo na kumpatia mkataba wa miaka miwili juzi Jumamosi (Januari 06), ukiwa ni usajili wa pili kufanywa na Simba SC baada ya kuanza kumtambulisha mshambuliaji kutoka Zanzibar, Saleh Karabaka.

Sarr mwenye urefu wa mita 1.83 aliyezaliwa Julai 24, 1997 katika mji wa Thies, Senegal amewahi kuzichezea tinu za Wallydann, AS Pikine, Mbour PC na Teungueth zote za Senegal kabla ya kutua Olympique Beja aliyotwaa nayo taji la Kombe la Tunisia msimu uliopita kabla ya kusajiliwa US Monastir aliyoichezea nmsimu huu.

Sarr aliwahi kucheza dhidi ya mshambuliaji wa Ureno, Cristiano Ronaldo katika mechi za michuano ya Klabu Bingwa ya Nchi za Kiarabu iliyopigwa Julai 31, mwaka jana kati ya Al Nassr dhidi ya US Monastir.

Katika mechi hiyo, Al Nassr ilishinda mabao 4-1, mabao ya Talisca dakika ya 42, Ronaldo dk 74, Alamii dk 88 na All-Aliwa dk 90, huku la US Monastir likifungwa na Alawjami aliyejifunga dakika ya 66.

Taarifa zinaeleza kuwa Benchikha amefurahia usajili wa kiungo huyo ambaye anasifika kwa uwezo mzuri wa kukaba, kuchezesha timu na kutembea na mpira kwa usahihi, jambo ambalo lilikuwa likimuumiza kichwa kutokana na Fabrice Ngoma na Sadio Kanoute wote kuwa wachezaji wa aina nyingine tofauti na aliyonayo Sarr.

Kocha alikuwva akihitaji kiungo mkabaji ambaye pia ana uwezo wa kufanya vitu vingine kama kutunza mpira na kutembea nao kwa usahihi mkubwa na baada ya kuletewa Sarr, kocha alifurahia kwa kuwa anamfahamu mchezaji huyo na uwezo wake mkubwa ulikuwa unamvutia hivyo amefurahi kumpata.

Kocha alikuwa akihitaii kiungo ambaye anaweza kukaba, kutembea na mpira pale ambapo wapinzani watakuwa wameubana uwanja na kwa namna moja ama nyingine Sarr anaweza hiyo kazi, hivyo amefurahia kuwa na kiungo mzuri kama huyo, wapo viungo wengine Simba SC ni wazuri lakini wengi wanafanana uchezaji wao tofauti na Sarr ambaye ndio alikuwa akimtaka,” kimesema chanzo hiko.

Kwa upande wa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema: Tumefurahi kumpata mchezaji mkubwa kweli kweli Barani Afrika, ni mchezaji mkubwa na tunafurahi kaja kucheza timu kubwa vilevile, hivyo ninachowaambia Wanasimba kwa sasa kwa kiungo huyo wasiwe na wasiwasi tena na timu yao.”

SOMA NA HII  SABABU MECHI ZA LIGI KUU KUTOTUMIA VAR