WAKATI Simba inashuka dimbali kesho katika fainali ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege, uongozi wa timu hiyo umefunguka kuhusu taarifa zinazomuhusu mshambuliaji wao, Kibu Denis kutakiwa na klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Kutokana na taarifa zilizozagaa kuwa klabu ya Mamelodi Sundowns imepeleka ofa Simba kuhusu kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa kwenye kwenye majukumu ya timu ya Taifa Stars ilipo nchini Ivory Coast katika fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Taarifa hiyo inadai kuwa klabu ya Mamelod Sundowns imetuma ofa kwa mara nyingine Simba kumuhutaji Kibu na kudaiwa uongozi wa Wekundu hao wapo kimya kuhusu kukubali au kukataa ofa yao.
Uongozi wa miamba ya mtaa wa Msimbazi umesema hawajapokea ofa kuhusiana na suala hilo la kutakuwa kwa mshambuliaji huyo na wapo katika mipango ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema katika meza ya klabu hiyo au yoyote kuhusu ofa inayohitaji huduma ya mchezaji wao huyo au mwingine kwa sasa wanafikiria kuimarisha kikosi cha timu yao ili kuongeza ushindani katika michezo iliyopo mbele yao.
Amesema mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya taarifa hizo hakuna taarifa aliyopokea kutoka kwa uongozi kuhusu kupokea ofa kutika klabu yoyote nje ya Tanzania kuhutaji huduma ya mchezaji wao Kibu au Willy Onana anayehusishwa na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.
“Hawa wachezaji wako kwenye mipango ya kocha wetu Abdelhak Benchikha, kwa sasa tunahitaji kuboresha kikosi cha timu kama ulivyoona tumeshatambulisha wachezaji wachezaji watatu akiwemo Salehe Karabaka, Babacar Sarr na Ladack Chasambi na hivi karibuni tutamtambulisha nyota mwingine.
Tunahitaji kuongeza mtu na hiki kipindi sio cha kuondoa wachezaji muhimu kwa kuuza kwa sababu ni muda wa kuboresha kama ilivyo kwetu tunaboresha timu kulingan na nafasi zilizopendekezwa,” amesema Ahmed.
Ameongeza kuwa uongozi umeamua kumuachia majukumu yake kocha Benchikha kwa kutoingilia mambo yake hasa katika kuhakikisha Simba inakuwa imara na wachezaji kujutuma kwa kupambania timu.
“Ni kweli kocha Benchikha ni mkali na huwa anahitaji mchezaji kufuata maelekezo yake kwa asilimia 100, ndio maana sasa hivi tunaona jinsi ya wachezaji wanavyojituma na kupambana uwanjani tofauti na ilivyo awali,” amesema Meneja huyo.
Mh