KUNA timu zinakimbizana kuzipata saini za mastaa waliotemwa na wanaotajwa kuachwa Simba na Yanga, kabla ya kufungwa kwa usajili wa dirisha Jumatatu Januari 15 saa 5:59 usiku.
Tayari baadhi yao wanatajwa wanaweza wakasaini muda wowote kuanzia sasa na wengine hawajafanya maamuzi wapi wanataka kwenda kufanya
DENIS NKANE – YANGA
Winga wa Yanga, Denis Nkane kuna asilimia kubwa anaweza akajiunga na Dodoma Jiji kwa mkopo, imeelezwa kocha Francis Baraza aliyewahi kumfundisha Biashara United ndiye anataka asainiwe.
Kwa upande wa Nkane alipoulizwa juu ya tetesi hizo, alisema “Mimi mwenyewe nasikia ila sijui chochote, ninachofahamu mimi ni mchezaji wa Yanga hadi 2025.”
NADO, LYANGA – AZAM
Wachezaji wa Azam Iddy Nado na Ayub Lyanga wanatajwa kutafutiwa timu kwa mkopo, kati ya timu zilizotajwa ni Singida Fountain Gate na Namungo.
Msimu uliopita Nado alikuwa na mabao saba, msimu huu ana mabao matatu, wakati Lyanga akiwa na bao moja (2023/24).