Home Habari za michezo WAKATI IVORY COAST ‘WAKINDEMA NDEMA’ AFCON…JINA LA PACOME LAIBUKA TENA HUKO….

WAKATI IVORY COAST ‘WAKINDEMA NDEMA’ AFCON…JINA LA PACOME LAIBUKA TENA HUKO….

Habari za Yanga leo

WAKATI mjadala wa kutojulikana kwa Pacome Zouzoua kwao Ivory Coast ukiwa unapamba moto kwa mashabiki kushambuliana, kocha Mfaransa aliyempandisha kiungo huyo amecheka kwa dharau kisha akafafanua kila kitu.

Kocha wa Asec Mimosas, Jullie Chevalier amesema kama kuna mtu ametamka Pacome hajulikani Ivory Coast hayo ni mawazo yake na sio watu wanaofuatilia soka la nchi hiyo hapo ndani.

Chevalier amesema anaheshimu mawazo ya watu lakini hawezi kukubaliana na hoja kwamba kiungo huyo hajulikani wakati ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini humo akiibeba Asec kwenye mashindano yote kabla ya kusajiliwa Yanga.

Kocha huyo alisema hatua ya kiungo huyo kujumuishwa kwenye kikosi cha taifa cha awali kuelekea fainali za Mataifa Afrika zinazofanyika nchini humo pia ni ishara ya ukubwa wa Pacome.

“Kama kuna mtu amesema hivyo labda hafuatilii mambo ya soka, sidhani kama amesema kitu sahihi juu ya Zouzoua kwa hapa Ivory Coast, watu wa hapa wanapenda soka sana angalia wanavyoumia na matokeo ya timu ya taifa, hao watu wanashindwaje kumjua mchezaji bora wa ligi hapa,” alihoji Chevalier na kuongeza;

“Nadhani alistahili kubaki timu ya taifa naona jinsi mashabiki hapa wanaumia na kikosi cha taifa hili licha ya kuwa na wachezaji wakubwa wanaoncheza Ulaya huu ni wakati wachezaji wanaocheza ligi ya ndani na hata hapoa Adrika kupewa nafasi pia.”

Kuna video ilisambaa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro akizungumza na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast na kumuulizia Pacome waziri huyo wa alibaki akishangaa na kuhoji Pacome ndio nani.

SOMA NA HII  KIGOGO WA SOKA AFRIKA AVUNJA UKIMYA..."YANGA INA NGUVU KUBWA SANA

4 COMMENTS