Home Habari za michezo ACHANA NA ISHU YA WACHEZAJI WA YANGA KUKATWA ….PANGA KUPITA TENA KWA...

ACHANA NA ISHU YA WACHEZAJI WA YANGA KUKATWA ….PANGA KUPITA TENA KWA MASTAA TAIFA STARS….

Taifa Stars leo

Mastaa wa Yanga, Nickson Kibabage na Abuutwalib Mshery wametemwa kwenye kikosi cha wachezaji 31 wa kikosi cha timu ya taifa kujiandaa na Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zinazotarajiwa kuchezwa Ivory Coast.

Akizungumzia kikosi alichobakinacho baada ya mchujo alisema haikuwa kazi rahisi kupunguza wachezaji anaamini wachezaji 31 waliobakia ambao pia atawachuja siku mbili mbele watakuwa na tija kubwa kwa taifa.

“CAF wanataka wachezaji 27 lakini sisi tunakwenda nchini Misri na wachezaji 31 lengo ni kuhakikisha tunakuwa na wachezaji wa ziada endapo wengine kati yao watapata majeraha kwenye maandalizi wataziba mapengo,”

31 WALIOITWA

Aishi Manula (Simba), Metacha Mnata (Yanga), Kwesi Kawawa (Karlslunds, Sweden), Beno Kakolanya (Singida Fountain Gate FC), Mohammed Hussein (Simba), Ibrahim Hamadi Bacca (Young Africans), Dickson Job (Young Africans), Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Sospeter Banyana (Azam FC), Feisal Salum (Azam FC), Novatus Dismas (Shakhtar Donesk, Ukraine).

Saimon Msuva (Js Kabylie, Algeria), Mzamiru Yasin (Simba), Mudathir Yahaya (Young Africans), Ben Starkie (Likeston Town, England), Miano Danilo ((Vilena, Spain), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Kibu Dennis (Simba), Mbwana Samatta (Paokm Solanika, Greece), Twaliq Abdillahi (Telford United, England).

Wengine ni Morice Abraham (RFK Novi, Serbia), Khleffin Hamdoun (Muscat Club, Oman), Himid Mao (Taka’ea El Gaish, Egypt), Abdul Suleiman Sopu (Azam FC), Banda, Haji Mnoga (Aldershot Town, England), Abdi Banda (Richardson Bay, South Africa), Cyprian Kachwele (Vancouver FC, Canada), Abdulmalik Zakaria (Namungo), Charles M’mombwa (Macarthur FC, Australia),Mohammed Ali Omar (Boreham Wood, England na Tarryn Allarakhia (Wealdstone, England).

Amrouche amesema kundi F walilopangwa sambamba na timu DR Congo, Morocco na Zambia anatambua wanaenda kukutana na timu bora na zenye majina makubwa lakini hawahofii hilo wamejiandaa kwenda kushindana.

“Tunakutana na timu nyingi ambazo zina mafanikio kwenye michuano hiyo lakini hayo ni mambo ya nyuma yalishapita tunaenda kuanza upya na Tanzania tukiwa miongoni mwa timu zilizopo kwenye ushiriki;

“Majina makubwa ya timu hizo hayatutushi tunajiandaa kwenda kushindana kwa upande wangu naamini katika mapambano siandai timu kwaajili ya kwenda kupata sare naenda kushinda na nina kikosi makini,”

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA WATATU CHAP....YANGA WAPANGA KUWAFANYIA 'UNYAMBISI' MASTAA WAKE WALIOBAKI...