NYOTA watatu wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze huenda wakaukosa mchezo dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 31.
Yanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United inayonolewa na Francis Baraza Uwanja wa Karume baada ya kumalizana na KMC kwa kuichapa mabao 2-1.
Wachezaji hao ni pamoja na Carlos Carlinhos ambaye anatibu jeraha lake la enka, Mapinduzi Balama pamoja Haruna Niyonzima ambaye anasumbuliwa na Malaria.
Kwa sasa timu ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwakila kitu kinakwenda sawa na wanatarajia kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushinani mkubwa.
Yanga ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake 19 inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya tatu kibindoni na pointi zake ni 16.