Home Habari za michezo FT:- YANGA 1-3 APR…..SIMBA NJIA NYEUPEEE….SHIBOUB AKUMBUSHIA ENZI….SKUDU CHALII…

FT:- YANGA 1-3 APR…..SIMBA NJIA NYEUPEEE….SHIBOUB AKUMBUSHIA ENZI….SKUDU CHALII…

FT:YANGA 1-3 APR

Yanga imekubali kipigo cha mabao 3-1 mbele ya APR ya Rwanda na kutupwa nje ya mashindano huku mashabiki wa watani wao Simba wakiwacheka wakisema wamewakimbia.

Matokeo hayo sasa yanaifanya APR kuwafuata mabingwa watetezi Mlandege FC ambaye mapema alitangulia kutinga nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 3-2 dhidi ya KVZ baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 wakiwa suluhu.

Ikitoka nyuma APR walifanikiwa kusawazisha bao na kuongeza mengine kisha kuupiga mpira mwingi kipindi cha pili kwa kuiweka kwenye wakati mgumu Yanga ikitengeneza pia nafasi nyingi.

Yanga ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 23 mfungaji akiwa winga Jesus Moloko akifunga kwa shuti Kali akipokea pasi safi ya mshambuliaji wake Clement Mzize ambaye kabla ya kutengeneza pasi hiyo ya bao akatangulia kumtoka beki wa APR akimzidi nguvu na mbio.

Yanga walitawala vizuri kipindi cha kwanza wakicheza soka lao la pasi za kutosha na kuwafanya APR kuwa kwenye wakati mgumu kwenye kipindi hicho Cha kwanza.

Wakati kipindi hicho Cha kwanza kikielekea mwishoni ndani ya dakika nne za nyongeza APR ikasawazisha bao mfungaji akiwa Soulei Sanda akimalizia vizuri mpira uliotemwa na kipa Aboutwalib Mshery kufuatia shuti la mshambuliaji Victor Mbaoma.

Bao hilo la APR lilitokana na makosa ya kiungo na nahodha wa mchezo huo kwa Yanga Zawadi Mauya alipoteleza na mpira kunaswa na mshambuliaji kisha akawatoka mabeki na kupiga shuti hilo, na kuifanya timu zote kwenda mapumziko wakiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili APR wakarudi na kasi ambapo dakika ya 49 wakafanikiwa kupata bao la pili mfungaji akiwa Mbaoma kwa mkwaju wa penalti baada ya Mshery kumchezea vibaya mchezaji wa wanajeshi hao wa Rwanda.

Wakati Yanga ikijapanga kusawazisha bao hilo wakajikuta wanapigwa bao la tatu mfungaji akiwa Sharaf Shaiboub aliyeingia kipindi cha pili akitumia pasi safi ya kisigino ya mshambuliaji Taiba Mbonyumwami.

SOMA NA HII  YANGA NA SIMBA... ZIMETUHAKIKISHIA KUPELEKA TIMU 4 KIMATAIFA MSIMU UJAO