Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA ENG HERSI KUALIKWA PSG….JEMEDARI SAIDI KAIBUKA NA HOJA HIZI...

KUHUSU ISHU YA ENG HERSI KUALIKWA PSG….JEMEDARI SAIDI KAIBUKA NA HOJA HIZI NZITO…

Habari za Yanga leo

Anaandika Jemedari Saidi kupitia ukurasa wake wa kijamii,Kwa mujibu wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam Rais wake Eng. Hersi Said ambaye pia ni Mwenyekiti umoja wa vilabu Afrika alialikwa na Rais wa PGS Nasser Bin Ghanim Al-Khaifi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu barani Ulaya.

Yanga imesema ni MUALIKO MAALUMU kwajili ya kujadili namna vyama wanavyoviongoza vitakavyofanya kazi kwa mashirikiano na kujenga uhusiano mzuri utakaosaidia maendeleo ya vilabu na wanachama.

Jambo jema sana hili ambalo nilitegemea Mwenyekiti wa vilabu vya Afrika angeongozana walau na wasaidizi, lakini kama aliamua kwenda peke yake pia hakuna ubaya.

Nikasema kwakuwa Rais wa PSG amempa “MUALIKO MAALUMU” Rais wa YANGA, kwa umaalumu huo huo PSG hawajaona umuhimu wa walau kupost picha za kikao hicho “MAALUMU” kwenye social media zao. Nimepita kuanzia Website ya PSG, Twitter (X), Instagram etc etc sijaona pahala ambako PSG hata wametamka lolote juu ya mualiko huu “Maalumu” au wao PSG jambo hili kwao sio MUHIMU kama ambavyo Yanga wamelifanya kuwa?

Wenye mawazo kama yangu wanaweza kudhani Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa vilabu Afrika alikwenda Paris kwenye shughuli zake akapita na Parc de princes kuona mechi dhidi ya Toulouse akapiga picha na kombe na wachezaji kisha akapata picha na Rais wa Klabu kitu ambacho kinawezekana hasa baada ya kujitambulisha vizuri ukiwa umefanya lobbing.

Kitu ambacho kinafanywa na watu wengi wanapokwenda ng’ambo matembezini na vilabu vya Ulaya vinataka kujitanua. Kitu kimoja kizuri nimeona video na KALIKONJI kapost Hersi anazungumzia Utalii, that was Great 👍.

Ila hili la “MUALIKO MAALUMU” itakuwa PSG hawakumpa heshima stahiki Mwenyekiti wa vilabu Afrika mpaka wametuibua sisi.

BIN KAZUMARI MTIPA (The voice of the voiceless)

SOMA NA HII  MASAA KADHAA KABLA YA KUIVAA YANGA...PABLO 'AWASUSIA WACHEZAJI MECHI'...AFICHUA ALICHOWAELEZA..

2 COMMENTS

  1. Kama ni rahisi na wewe nenda Paris tena kaonane na President wa PSG piga nae picha kisha uje utupostie kwenye mitandao. binafsi sijaona umuhimu ya article yako, imekaa kisiasa Sana. Mbona hukufanya mahojiano na Eng? Hii ni Sawa na kumsema marehemu, ukisikia matumizi mabaya ya karamu ndo kama hivi umefanya.