Home Habari za michezo “KELVIN JOHN HASTAHILI KUJIITA MBAPPE….KWANZA ANADHARAU NA NIDHAMU MBOVU”….

“KELVIN JOHN HASTAHILI KUJIITA MBAPPE….KWANZA ANADHARAU NA NIDHAMU MBOVU”….

Habari za Michezo leo

WAKATI wadau wengi wakihoji kukosekana kwa jina la mshabuliaji wa KRC Genk, Kelvin John kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kinachoenda kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) kocha mkuu wa timu hiyo Adel Amrouche amefunguka sababu.

Amrouche amefunguka hayo saa chache kabla ya kuondoka kwenda Misri kwa ajili ya kambi ya timu ya taifa alisema nidhamu mbovu aliyonayo ndiyo imemuengua kikosini.

Alisema ni mchezaji mzuri endapo atabadilika na kuamua kuwekeza nguvu kiwanjani huku akiupa mchezo huo heshima kwa kuwa na nidhamu bora kiwanjani na nje ya uwanja.

“Sijaita kikosi kwasababu ya mtu fulani hiki ni kwa ajili ya Tanzania, hivyo Tanzania kwanza, natambua uwezo wa mchezaji huyo ni mzuri natakiwa kumlinda na kukuza uwezo wake nitafanya hivyo endapo atabadilika;

“Hapaswi kulinganishwa na Mbappe, Mbappe ni mchezaji mkubwa ni nahodha wa timu yake ya taifa amekuwa akilipambania taifa lake pale Ufaransa, huyo Kelvin anatakiwa kubadilika na kupambania nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza siwezi kuacha wachezaji ambao wanacheza nikamchukua mchezaji anatokea benchi na ananidhamu mbovu,” alisema

SOMA NA HII  ACHANA NA SABABU ZA VIJIWENI..HUU HAPA UKWELI WA SIMBA NA YANGA KUANZIA HATUA YA AWALI KLABU BINGWA AFRIKA...