Home Habari za michezo USAJILI MPYA WAANZA NA BALAA ZITO SIMBA…PHIRI AKIANZA ‘KUJISHTUKIA’ MDOGO MDOGO…

USAJILI MPYA WAANZA NA BALAA ZITO SIMBA…PHIRI AKIANZA ‘KUJISHTUKIA’ MDOGO MDOGO…

Habari za Simba leo

Mchezo  wa kwanza kwa Simba wa michuano ya Mapinduzi waliocheza dhidi ya JKU katika Uwanja wa New Amaan Complex umemalizika kwa ushindi wa mabao 3-1.

Moses Phiri alifunga bao la kwanza dakika ya nane baada ya kupokea ya pasi safi kutoka kwa Luis Miqussone.

Mshambuliaji Neva Kaboma aliisawazishia JKU bao hilo dakika ya 42 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Simba na kupiga shuti lililomgonga Che Malone na kumchanganya mlinda mlango Ayoub Lakred.

Mohamed Hassan wa JKU alijifunga na kuipatia Simba bao la pili dakika ya 64 katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Miqussone.

Saleh Karabaka alifunga bao la tatu dakika ya 65 muda mfupi baada ya kuingia na kupiga shuti liliomshinda mlinda mlango Enock Gerard.

Itakumbukwa pia Simba imemsajili wa kiungo, Saleh Karabaka kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka mitatu.

Usajili wa Karabaka mwenye umri wa miaka 23 unakuwa wa kwanza katika dirisha hili dogo kwa upande wa Simba SC.

Pamoja na uwezo alionao Karabaka jambo jingine lililowavutia Simba ni umri wake mdogo ambao wanaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu yao.

X1: Lakred, Kapombe, Duchu, Kazi, Che Malone, Ngoma, Mwanuke (Onana 45′), Kanoute, Chilunda (Mussa 45′), Phiri (Baleke 45′), Miqussone (Kalabaka 64′)

Walioonyeshwa kadi:

X1: Enock (Haji Ally 69′), Yakubu (Ubwaka 55′), Suwed, Mohamed, Shaban, Hassan (Antwi 68′), Saleh, Adam, Nassor, Ahmed (Machano 56′), Neva

Kazi 16′ Chilunda 27′

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE