Home Habari za michezo SAKHO AFICHUA TABIA ZA SARR NNJE YA UWANJA …ATAJA USTARABU, DHARAU NA...

SAKHO AFICHUA TABIA ZA SARR NNJE YA UWANJA …ATAJA USTARABU, DHARAU NA KUJIONA….

Habari za Simba leo

SIMBA tayari imemtambulisha kiungo mkabaji Msenegal, Babacar Sarr na jana usiku aliingia kipindi cha pili kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamuhuri, Mnyama ikishinda bao 1-0 kwenye Uwanja wa New Amaan Cmplex.

Sarr amesajiliwa kama mchezaji huru akitokea US Monastir ya Tunisia, lakini licha ya kiwango chake bora kilichoivutia Simba pia tabia zake nje ya uwanja unaambiwa ni mtulivu na asiye na makuu.

CV ya jamaa ni kubwa, kingine kinachowavutia mashabiki wa Simba ni kuwahi kumkaba Cristiano Ronaldo wa Al Nassr na aliyekuwa winga wa Simba, Pape Ousmane aliyewahi kucheza na Sarr Teungueth ya Senegal, ameelezea nje ya uwanja jamaa ni mtu wa aina gani.

“Sarr sio mwongeaji, hivyo wachezaji wa Simba wasije wakamwona anajisikia ama ni mtu fulani anayevimba, ila ni mtu mstaarabu sana na anayependa wengine afanikiwe,” amesema na kuongeza,

“Hakurupuki kwenye kuzungumza vitu mbele ya watu, mvumilivu wa kumsikiliza mtu, akiwa na cha kushauri anakuita na kukwambia kitu gani kinafaa, wapi na muda gani.”

Mchezaji mwingine aliyecheza na Sarr ni kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Gibril Sillah, pia kamzungumzia kiungo huyo itamchukua muda mfupi kuzoea mazingira, ila baada ya hapo mashabiki watajivunia mchezaji huyo.

“Jamaa ni mpole sana, anajua kuweka muda wake kwenye vitu vya msingi, kuhusu mazingira yatampa shida kwa muda mfupi, kwani hata mimi nimeyapitia hayo,” amesema na kuongeza;

“Jambo lingine anapenda sana kujali muda kuanzia kwenye kula, kupumzika, mazoezi, kifupi anajua kitu gani anakitaka kwenye kazi yake.”

SOMA NA HII  KOCHA WA VIUNGO SIMBA AFUNGUKA JINSI ALIVYOPATA ZALI LA KUAJIRIWA...ATOA SABABU ZA KUKATAA OFA ZA WAARABU...