Home Habari za michezo HESABU ZA GAMONDI NA YANGA ZIMEKAA HIVI BAADA YA LIGI KUSIMAMA…

HESABU ZA GAMONDI NA YANGA ZIMEKAA HIVI BAADA YA LIGI KUSIMAMA…

Habari za Yanga leo

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga hesabu zake kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye mashindano makubwa matatu ambayo wanashiriki baada ya Mapinduzi 2024 kugota mwisho.

Ipo wazi kuwa Yanga iligotea hatua ya robo fainali Mapinduzi 2024 ubingwa ukibaki kwa mara nyingine mbele ya Mlandege waliupata ushindi wa bao 1-0 Simba kwenye mchezo wa fainali iliyochezwa Januari 13 2024.

Gamondi ameweka wazi kuwa vita nyingine uwanjani ya kusaka ushindi inaendelea kwenye Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam Sports Federation.

Gamondi amesema kuwa kila mashindano ambayo wanashiriki ni muhimu kufanya vizuri na kikubwa ni kupata ushindi uwanjani.

“Kwenye mashindano ambayo tunashiriki ni muhimu kupata ushindi kwa kuwa kila mchezo tunahitaji kupata matokeo. Wachezaji wanalitambua hilo hivyo tunafanyia kazi makosa yaliyopita ili tuwe imara.

“Makosa yaliyopita tunafanyia kazi sehemu ya mazoezi hilo linatufanya tuzidi kuwa imara kwa kupunguza zaidi makosa kwenye mechi,”.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA NA YANGA LEO....KIBARUA CHA PABLO KIPO REHANI SIMBA....MUDA WOWOTE 'KITANUKA' HUKOO...