Home Habari za michezo KISA MECHI NA MISRI JUZI…AMROUCHE “AKUNA KICHWA” VIWANGO VYA MASTAA TAIFA STARS…

KISA MECHI NA MISRI JUZI…AMROUCHE “AKUNA KICHWA” VIWANGO VYA MASTAA TAIFA STARS…

Taifa Stars

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Stars, Adel Amrouche amesema bado ana kazi ya kufanya kwa wachezaji wake wote kucheza kwa uwiano mzuri kabla ya mchezo wao wa kwanza wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Morocco.

Kauli ya kocha huyo ni baada ya mchezo wa kwanza wa kirafiki waliocheza juzi dhidi ya timu ya Taifa ya Misri na Stars kukubali kichapo cha mabao 2-0, nchini Misri kabla ya jana kuondoka kuelekea Ivory Coast kwa ajili ya fainali hizo.

Stars tayari imewasili katika mji wa San – Pedro ambapo watacheza mechi ya kwanza ya makumdi ya Fainali za AFCON zinatarajiwa kuanza Januari 13 hadi Februari 11 mwaka huu nchini Ivory Coast na Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Morocco na Zambia.

Kocha Mkuu wa Stars, Amrouche alisema mechi ilikuwa mzuri na kipimo cha timu yake lakini hakufurahishea na baadhi ya kiwango kilichoonyeshwa na baadhi ya wachezaji wake.

Alisema ameona makosa katika kikosi chake na kunakikisha anafanya kazi haraka ndani ya siku nane zilisalia kabla ya kucheza mechi yao ya makundi ya fainali hizo dhidi ya Morocco.

“Ninajua kile tulichonacho, lazima tukubali na uhalisia , kuna baadhi ya wachezaji wamecheza chini ya kiwango, nilichotegemea, huu ndis ukweli na sote tumeona.

Tunahitaji wachezaji wanaoweza kufanya kitu , nimefurahishwa na baadhi yao akiwemo Tshabalala (Mohammed Hussein) kurudi katika ubora wake lakini sijafurahishwa pia na kiwango cha wengine,” alisema Amrouche.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema mchezo ulikuwa mzuri na kuwapa ushindani mkubwa kwa sababu ya ubora wa kikosi cha timu ya Taifa ya Misri, ikiwa na kikosi cha wachezaji bora na wazuri.

Alisema mchezo ulikuwa kipimo kizuri na kumpa nafasi kocha kufanyia kazi mapungufu ya kikosi cha timu hiyo kabla ya kuanza kwa fainali za AFCON .

“Kocha ameona maeneo ya kufanyia marekebisho, atajaribu kuandaa timu kuona kiwango tulichokionyesha leo (jana), maeneo tuliokuwa mazuri na nini kinatakiwa kuongeza na wapi kutumia makosa ya mpinzani ili kupata matokeo mazuri katika mechi yetu ijayo dhidi ya Morocco,” alisema Samatta.

Stars itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwenye fainali hizo Januari 17 dhidi ya Morocco na kisha Januari 21Januari 21 dhidi ya Zambia utachezwa katika mji wa San – Pedro na Januari 24. DR Congo,

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA LEO....NABI ATAMBA NA REKODI YA DABI SITA ZA NYUMA....ZORAN KAMTAZAMA KWA JEURI KISHA AKAMJIBU HAYA...