Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA ONANA KUTAKIWA NA WAALGERIA….SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI RASMI…

KUHUSU ISHU YA ONANA KUTAKIWA NA WAALGERIA….SIMBA WAIBUKA NA TAMKO HILI RASMI…

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba umesema hawajapokea barua kutoka klabu ya JS Kabylie ya Algeria au timu yoyote inayomuhutaji huduma ya kiungo wao mshambuliaji, Willy Essomba Onana na kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo.

Hauli hiyo ni baada ya taarifa kuwa JS Kabylie wameonyesha nia ya kutaka kumsajilu nyota kutoka kutoka Simba, wanamtaka kiungo huyo kuchukuwa nafasi ya Simon Msuva ambaye waliachana naye hivi karibuni.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema hajapokea taarifa zozote kutoka kwa viongozi wake juu ya klabu hiyo kupelekea ofa na kumtaka mchezaji wao huyo.

Amesema kulingana na jinsi ya ilivyo kwa kikodi chao wanaendelea kujenga kikosi na mchezaji huyo ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwa kipindi chote cha mkataba wake.

“Kwa sasa Onana ni mali ya Simba hakuna ofa iliyofika mezani kwetu kutoka hiyo klabu ya JS Kabylie, kwa sasa sio rahisi kumtoa mchezaji ambaye ameingia katika mfumo wa mwalimu na huku tunaongeza watu kuboresha timu yetu,” amesema Ahmed.

Amesisitiza kuwa baada ya kutambulishwa kwa wachezaji wawili mbao tayari wamewasajili bado wanaendelea kushusha vifaa vipya waliowasajili kipindi cha dirisha dogo ikiwa sehemu ya maboresho ya timu yao.

Ameeleza kuna usajili unaendelea kufanyika na wanatarajia kutambulisha nyota wawili ndani ya wiki hii kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Abdelhak Benchikha.

SOMA NA HII  NABI AFUNGUKA ISHU YA 'KUMSUSA' MAYELE JUZI...SABABU NYUMA YA PAZIA NI HIZI HAPA..