Home Habari za michezo UNAAMBIWA SARR ALIWACHANIA SIMBA MKATABA MARA TATU….ISHU NZIMA IKO HIVI….

UNAAMBIWA SARR ALIWACHANIA SIMBA MKATABA MARA TATU….ISHU NZIMA IKO HIVI….

Habari za SIMBA LEO

UNAAMBIWA kama kuna dili limewatingisha mabosi wa Simba basi ni mkataba wa kiungo mpya wa timu hiyo, Babacar Sarr ambaye amekuwa staa wa kwanza wa kigeni kusaini mkataba katika dirisha hili dogo la usajili.

Hata hivyo, Simba imefichua kwamba haikuwa kazi rahisi kumsainisha mkataba kiungo huyo wa zamani wa US Monastir ya Tunisia aliyewahi kumkaba, Cristiano Ronaldo na anayecheza nafasi ya ukabaji baada ya kuwavuruga hasa mabosi wa klabu hiyo wakati wa mazungumzo.

Bosi mmoja wa juu wa Simba ameliambia Mwanaspoti, Sarr aliwarudishia mkataba mara tatu akitaka maboresho makubwa ambayo atakubaliana nayo vinginevyo asingesaini dili hilo.

Simba imekiri kuwa raia huyo wa Senegal ni staa mkubwa ambaye anajua kusimamia haki zake huku mambo yote akiyaamua mwenyewe na mwanasheria wake.

Hata hivyo, Simba ikafanikiwa kupangua ugumu huo na kumalizana naye jamaa akisaini mkataba wa miaka miwili kuvaa jezi nyekundu na nyeupe.

“Haikuwa rahisi kabisa jamaa ni mtata sana anajua kusimamia haki zake kisawasawa tumetumia kama wiki tatu hivi kujadiliana. Kuna wakati tunapishana kuna wakati tunakuja kuelewana,” alisema bosi huyo wa juu ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba.

“Ilifika wakati tuliona kama tutakata tamaa maana kuna mambo alikuwa anayataka sasa huku kwetu huwa hatutoi kwa wachezaji lakini tulielewa baadaye kwamba huyu ni mchezaji aliyepita klabu kubwa na amecheza na wachezaji wakubwa.”

AANZA TIZI

Sarr jana alianza mazoezi rasmi na Simba yakiwa ndio mazoezi yake ya kwanza na wekundu hao tangu asajiliwe juzi.

Kiungo huyo mwili jumba tayari alishawasili kisiwani hapa na kukutana na kocha Abdelhak Benchikha.

SOMA NA HII  SIMBA YATINGA MAKAO MAKUU,DODOMA,KUIBUKIA BUNGENI