Home Habari za michezo UTATA WA KONA YA SIMBA JUZI: GOLIKIPA SINGIDA FG AFUNGUKA KUDAKIA MPIRA...

UTATA WA KONA YA SIMBA JUZI: GOLIKIPA SINGIDA FG AFUNGUKA KUDAKIA MPIRA NNJE YA UWANJA…

Habari za Michezo

Wakati kelele zikiendelea kuwa nyingi juu ya shambulizi la kona katika mchezo wa Singida Fountain Gate dhidi ya Simba wadau watofautiana.

Kipa wa Singida Fountain Gate Ibrahim Parapanda amesema mwamuzi Nasri Salum ‘Msomali’ hakufanya maamuzi ya haki kwa kuwapa shambulizi la kona Simba kwa kuwa wakati anaudaka mpira tayari ulishakuwa umetoka.

Parapanda amesema wakati Msomali anaamua kuwa kona tayari mwamuzi wa kwanza msaidizi alitofautiana naye akisema mpira umetoka na upigwe kuelekea Simba.

“Namshangaa sana Msomali kwa kile alichoamua, kwanza ujue Mimi alishanionya kwamba nisipoteze muda, kwahiyo ule mpira wakati Saido (Said Ntibazonkiza) anaupiga haukumgusa mchezaji wetu yoyote na mimi nimeudakia nje ili nisipoteze muda tupige haraka kwa kuwa alishawaongezea sana muda,”amesema kipa huyo.

“Nikamwambia amuangalie hata msaidizi wake ameweka tupige sisi akawa hataki kutusikiliza akasimamia maamuzi yake, yule beki wa Simba Hussein Kazi alijua kwamba ule mpira ukitoka hautakuwa kona ndio maana alikuwa anataka kuuwahi usitoke haya yote hakutaka kuyaona kama yangemsaidia basi hata angekwenda kwa msaidizi wake amsikilize hakutaka,”

Naye kocha msaidizi wa Singida Nizar Khalfan amesema hata kama muda ulipotezwa lakini haukuwa kwa kiwango ambacho Msomali aliongeza huku pia akiwatupia lawama wapangaji wa waamuzi hao kwa hatua ya kumpanga mwamuzi huyo kwenye mechi zao zote mbili

“Sisi kwenye mashindano haya tumekutana na Simba mara mbili na mara zote kapewa mwamuzi huyu huyu tuanze kujiuliza Yuko peke yake? Angalia ile kona aliyowapa, hata kama muda ulipotezwa sio kwa kiwango ambacho aliongeza ikionyesha wazi kwamba alikuwa na hesabu zake.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA UBINGWA WA LIGI NA ASFC...NABI KAAMUA 'KUWAPA MAKAVU LIVE' MASTAA WAKE...