Home Uncategorized AZAM FC WAJA NA MBINU ZA KIBINGWA

AZAM FC WAJA NA MBINU ZA KIBINGWA


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam FC, Aristica Cioaba, amezikalia kooni Klabu za Simba na Yanga katika vita ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2020/21, baada ya kuamua kutambulisha mifumo ya kibingwa kwenye kikosi chake.

 

Azam ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi 15, baada ya kushinda michezo yote mitano iliyopita. Kikosi hicho kimetupia jumla ya mabao tisa na kumefungwa mabao mawili.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC Zakaria Thabith ‘Zaka za Kazi’ amesema Cioaba ametambulisha program maalum kwenye mazoezi ya timu hiyo.

 

“Tunashukuru Mungu kwa mwanzo mzuri wa ligi ya msimu huu ambapo ukiachana na ukweli kwamba hatujapoteza mchezo mpaka sasa. Tuna mtu wa kazi ambaye anajua kufunga na uwezo wake unaonekana ni Prince Dube.

 

“Kazi ni kubwa ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa nasi tunapambana kuwa tofauti na kupata matokeo mazuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.


Mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikamilika kwa Azam FC kutupia mabao 4-2 unashikilia rekodi ya kukusanya mabao mengi ndani ya dakika 90 kwa msimu wa 2020/21 ambapo ulikusanya jumla ya mabao 6.

SOMA NA HII  KIUNGO MPYA SIMBA AKOMBA MILIONI 138