Home Habari za michezo WAKATI AFCON IKIRINDIMA …..GAMONDI AANZA ‘KUZIMISI SHOW’ ZA KIMATAIFA YANGA….

WAKATI AFCON IKIRINDIMA …..GAMONDI AANZA ‘KUZIMISI SHOW’ ZA KIMATAIFA YANGA….

Habari za Yanga SC

KOCHA mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewaambia mabosi wa timu hiyo wafanye kila wanaloweza apate mchezo wa kirafiki kabla ya kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mapumziko ya kupisha fainali za Mataifa ( Afcon)kumalizika.

Gamondi ametoa kauli hiyo kufuatia kuendelea na programu za mazoezi na wachezaji wake wote ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa zinazoshiriki Afcon licha timu nyengine kuendelea na mapumziko.

Gamondi amesema kuna kila sababu ya timu yake kupata Michezo ya kimataifa ya kirafiki wakati huu wa mapumziki ili kujua ubora wa kikosi chake kwa kupata muunganiko ukiwemo wa wachezaji wapya kabla ya kurejea kwenye michuano ya kimataifa.

Amesema wanaendelea na mipango yao kwa sababu bado kazi kubwa ipo mbele yetu na wachezaji baadhi walikuwa kwenye mapumziko mafupi hawakuwepo katika Kombe la Mapinduzi

“Tumerejea mapema kuweza kujipanga kwa muda huu ambao upo kwa Sasa lakini wapo wapya ambao wameingia wanahitaji kuzoea timu ili tufikie malengo lazima tucheze mechi za kirafiki wakati huu ligi imesimama na ikiwezekana kama tutapata za kimataifa na nyengine za ndani.

Kwa sababu tunalenga kuboresha timu yetu kwa malengo ya kufanya vizuri kimataifa na wachezaji waliongia waweze kwenda sawa na waliokuwepo katika majukumu ya timu za Taifa,” amesema Kocha huyo.

Naye Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema baada ya mazoezi ya wiki moja katika sehemu mbalimbali ikiwemo ufukweni, Gym na uwanjani, mapema wiki hii kutakuwa na mechi za kirafiki .

Amesema kocha Gamondi amehutaji kuona timu yake kwa kuomba mechi ya kirafiki kuona wachezaji wake wapya waliosajili kipindi cha dirisha dogo na waliokuwepo tangu awali.

“Mashabiki wasiwe na wasiwasi timu ipo katika mazoezi na wiki hii wataiona Yanga yao, ikiwemo wachezaji wetu wapya akiwemo mtaalamu wa kutikisa nyavu kutoka Ivory Coast Joseph Guede, Pacome Zouzoua, Khalid Aucho na wengine ambao hawako katika majukumu ya timu za Taifa,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  PAMOJA NA JANA KUMSHAMBULIA BARBARA...SIMBA WAZIDI KUMKAZIA MORRISON..."KILA KITU KIPO KWENYE MAANDISHI"...