Home Habari za michezo GAMONDI:- HAWA AL AHLY HAWATAAMINI….NIACHIENIE ‘SHOW’ MWENYEWE KWENYE HILI…

GAMONDI:- HAWA AL AHLY HAWATAAMINI….NIACHIENIE ‘SHOW’ MWENYEWE KWENYE HILI…

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, ametaja sababu za kushinda magoli 4-0 dhidi ya CR Belouizdad na kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi ametoa kauli hiyo baada ya Jumamosi, kikosi cha timu yetu ya Young Africans SC kuibuka na ushindi huo mnono katika mchezo wa Kundi D uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kufuzu moja kwa moja robo fainali huku kukiwa na mechi moja mkononi.

Baada ya mchezo huo, Gamondi amesema kikubwa kilichosababisha ushindi huo, ni namna ya ufahamu wake mkubwa wa kucheza dhidi ya timu za Kiarabu kwani katika maisha yake ya kufundisha soka, amefundisha soka zaidi ya miaka 15 ndani ya Bara la Afrika.

“Ninajisikia furaha, kwanza kabisa naweza kusema hongera kwa Wananchi na wachezaji wa Young Africans kwa sababu tumeonesha kiwango kisichotarajiwa mbele ya timu kubwa kama CR Belouizdad, kiwango cha leo ni kizuri sana.

“Kitu kizuri ni kwamba tumefuzu, hata kama tukipoteza mchezo wa mwisho na wao (CR Belouizdad) wakashinda, tunakuwa tumepita kwani sisi ni bora zaidi yao kwa matokeo.

“Tumeweka historia ndani ya Young Africans, baada ya miaka 25 bila ya kufuzu, tukakubaliana na Rais (Eng. Hersi Said) kupambana hatua ya makundi, hatukuanza vizuri kutokana na ugumu wa kundi katika michuano hii ya CAF Champions League, lakini tukapambana.

“Wapo waliotukatia tamaa baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kisha kutoka sare, lakini ndani ya Young Africans, hakuna kukata tamaa, na leo imetimia, ama kwa hakika nina furaha sana.

“Kushindwa kufunga magoli mengi kipindi cha kwanza haimaanishi kwamba hatukucheza vizuri, bali wapinzani wetu nao walikuwa wakijilinda ili wasiruhusu kufunga magoli mengi.

“Kipindi cha pili tulivyorudi tukaja na nguvu nyingine na morali, tukatengeneza mazingira ya kupata magoli mengi, katika mpira wa miguu vitu kama hivyo huwa vinatokea. Kile tulichozungumza kinabaki kuwa siri yetu.

“Siku zote timu yangu ninataka ishinde bila ya kujali tunacheza dhidi ya nani, kama utakumbuka mechi dhidi ya Al Ahly tuliyocheza hapa kipindi cha kwanza ni sawa na ilivyokuwa leo, tulitawala mchezo, tukatengeneza nafasi, tulicheza vizuri.

“Binafsi ninazifahamu vizuri sana timu za Kiarabu, zaidi ya miaka 15 nimefundisha Afrika, hivyo nina kumbukumbu jinsi ya wao wanavyocheza, wanavyofikiria na wanachofanya. Kwa sasa tumetulia, tunafurahia, tunakwenda kupambana kuifunga Al Ahly, hakuna shida yoyote.”

SOMA NA HII  YANGA YAENDELEA KUNG'ANG'ANIA UBINGWA WA LIGI KUU BARA