Home Habari za michezo RASMI…MASTAA WATANO SIMBA KUIKOSA SAFARI YA KUWEKA KAMBI MISRI…SABABU KUU NI HIZI...

RASMI…MASTAA WATANO SIMBA KUIKOSA SAFARI YA KUWEKA KAMBI MISRI…SABABU KUU NI HIZI HAPA….


MASTAA watano wa kikosi cha Simba wataachwa Bongo kwa ajili ya kuweza kutimiza majukumu yao kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stasr.

Kikosi cha Simba leo Julai 14,2022 kinatarajiwa kukwea pipa kueleka nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wale ambao watakuwa kwenye Timu ya Taifa hawatajumuishwa kwenye msafara.

“Tutaondoka Julai 14 na wachezaji wetu wote lakini wale ambao wataitwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania hao watabaki kwa ajili ya maandalizi kisha wakikamilisha mechi watapata muda wa kujiunga na timu kambini,” amesema.

Wachezaji wa Simba ambao wameitwa katika timu ya taifa ni watano wanatarajiwa kuiingia kambini kujiandaa na michezo ya kufuzu CHAN.

Ni Aishi Manula ambaye ni kipa namba moja, Mohamed Hussein na Kennedy Juma hawa ni mabeki na

Mzamiru Yassin ambaye ni kiungo huku mshambuliaji akiwa ni Kibu Denis.

SOMA NA HII  GEITA GOLD WANOGEWA NA DUCHU...MIKAKATI YAFANYWA KIMYA KIMYA KUEPUSHA SHARI ZA SIMBA NA YANGA...