Home Habari za michezo KWA YANGA HII….TARAJIENI LOLOTE KUBWA MSIMU HUU KIMATAIFA…TAKWIMU ZAO SIO POA…

KWA YANGA HII….TARAJIENI LOLOTE KUBWA MSIMU HUU KIMATAIFA…TAKWIMU ZAO SIO POA…

Habari za Yanga leo

Yanga ya Gamondi ina wachezaji wenye ubora, uwezo na viwango vya Kimataifa, kisha wanacheza kwa kujituma sana. Wachezaji wa Yanga wana kiu ya mafanikio baada ya kubezwa kwa miaka mingi.

Tangu kuingia kwa uongozi wa Injinia Hersi Said, kuna mbegu flani ya kujituma na mafanikio ambayo ameipandikiza kuanzia kwa viongozi wa juu, wachezaji, benchi la ufundi na hata mashabiki na wanachama wao.

Miaka ya nyuma haikuwa rahisi kwa timu hasa za Tanzania kuwafunga Waarabu, leo hii kimekuwa kitu cha kawaida, Yanga wanapata matokeo sio tu kwenye uwanja wao na hata wakitoka nje ya mipaka ya Tanzania wanakuwa hawana presha, winning team siku zote haichagui uwanja wa kupigana vita.

Yanga wapo tayari kucheza na timu yoyote kwenye hatua zinazofuata kwa sababu wana uhakika na kikosi chao na kimekuwa kikiwapa matokeo chanya kwa miaka mitatu sasa.

Kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 25 Yanga anafanikiwa kutinga hatua ya makundi ya CAFCl na kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1969 na mwaka1970 walipoingia robo fainali ya michuano ya African Cup of Champions Clubs.

Mwaka 1995 wakaingia tena robo fainali CAF Cup Winners’ Cup na mwaka jana 2023 wakamaliza nafasi ya pili baada ya kucheza fainali ya CAF Confederation Cup.

Full — Yanga 4 – 0 Belouizdad

⚽️ Mudathir Yahya Abbas— 43′
⚽️ Stephanie Aziz Ki — 46′
⚽ Musonda Kennedy — 48′
⚽️ Joseph Gnadou Guede — 84′

Yanga na Al-Ahly wametinga robo fainali CAF-CL, watacheza Mchezo wa mwisho kutafuta kinara wa group.

1. Mechi 5, GD⚽ +4, Alama 9 — Al-Ahly
2. Mechi 5, GD⚽ +4, Alama 8 — Young Africans
3. Mechi 5, GD⚽ -2, Alama 5 — CR Belouizdad
4. Mechi 5, GD⚽ -6, Alama 4 — Medeama

Timu zilizofuzu hatua ya Robo Fainali ya CAF CL hadi sasa.

✅ Petro Luanda – Angola
✅ ASEC Mimosas – Ivory Coast
✅ TP Mazembe – Congo DR
✅ Al Ahly – Misri
✅ ⁠Mamelodi Sundowns – Afrika Kusini
✅ ⁠Yanga SC – Tanzania.

SOMA NA HII  SIMBA WAKOMBA MZIGO WOTE WA YANGA KUTOKA KWA RAIS SAMIA...ISHU YOTE IKO HIVI...