Home Habari za michezo KUHUSU KUIFUNGA JWANENG …SHABIKI SIMBA AMLIPUA AHMED ALLY…”ANATUDANGANYA HUYU”…

KUHUSU KUIFUNGA JWANENG …SHABIKI SIMBA AMLIPUA AHMED ALLY…”ANATUDANGANYA HUYU”…

Habari ya Simba leo

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa timu yao haina uwezo wa kuwafunga Jwaneng Galaxy kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.

Mchome amesema hayo kuelekea mchezo wa mwisho wa makundi kati ya Simba na Jwaneng utakaopigwa Jumamosi huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya kuondolewa na Jwaneng kwenye hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa mwaka 2021/22 hapo hapo Kwa Mkapa kwa kufungwa mabao 3-1.

“Jwaneng Galaxy na Simba ndiyo wana hali ngumu kwenye kundi lao kwa sababu uwezekano wa Wydad kupita kwa alama 9 anao. Wydad anamaliza na ASEC Mimosas ambaye tayari ameshafuzu na anaongoza kundi.

“Sisi Simba tumejiaminisha kwa kuposti makanuni, lakini Jwaneng Galaxy akimfunga Simba na ASEC akamfunga Wydad, bado Jwaneng atakwenda robo, kwa hiyo sio mchezo rahisi kama msemaji anavyotuaminisha kwa kuposti makanuni, kama vile ana uhakika.Hawa watu wana matatizo, wana stress.

“Jwaneng Galaxy tulienda kwao Botswana tukampiga 2-0, tukajiaminisha kuwa tumeshafuzu, akaja hapa akatuua 3-1 Kwa Mkapa, akafuzu kwa kanuni ya idadi ya mabao ya ugenini. Sasa hivi hatujamfunga Jwaneng tumetoa nae sare, huo jeuri ya kusema unafuzu unautoa wapi? Na kuanza kuposti kanuni za pointi 9?

“Msemaji anatuingiza chaka, Jwaneng Galaxy anaweza kutuua tena hapa, ana quality ya kutuua Kwa Mkapa. Kwa Simba hii ikipelekwa moto, Jwaneng anatoboa. Natoa ahadi tena, Simba ikishinda mbele ya Jwaneng Galaxy Kwa Mkapa, prize ihusike,” amesema Mchome.

SOMA NA HII  SIMBA, YANGA NA AZAM ZAPEWA KAMSELELEKO MICHUANO YA CAF...MBINU ZOTE ZA USHINDI SASA WAZI...MAKI AONYWA...