Home Habari za michezo MKOMBOZI WA YANGA ATUA BONGO….GAMONDI MENO YOTE NNJE…

MKOMBOZI WA YANGA ATUA BONGO….GAMONDI MENO YOTE NNJE…

Habari za Yanga

Hatimaye kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephanie Aziz KI amewasili nchini na jana akashtua akifika makao makuu ya klabu hiyo huku kocha wake Miguel Gamondi akimuita fasta mazoezini.

Gamondi ingawa timu yake imekuwa ikishinda kwa ushindi mwembamba wala hana shida na hilo amesema anafahamu siri kuhusu ugumu wanaokutana nao huku akikiri kuwa pengo la Aziz Ki lilikuwa wazi.

Aziz Ki amewasili nchini usiku wa kuamkia jana kimyakimya sambammba na kipa namba moja wa klabu hiyo Djigui Diarra ambao wote walikuwa wachezaji wa mwisho kutolewa kwenye Fainali za Mataifa Afrika.

Mara baada ya Aziz kufika haraka Gamondi alimuita mazoezini jana akitaka kuanza kupimwa juu ya utimamu wake wa mwili kabla ya safari yao ya jana usiku Yanga ikiifuata Prisons ya Mbeya.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gamondi alisema kwa taarifa alizopewa na mabosi wake ni kwamba Aziz Ki atakuwapo kwenye kikosi chao kitakachocheza dhidi ya Prisons kesho kwenye Uwanja wa Sokoine.

Kocha huyo, ambaye ameirudisha Yanga juu ya msimamo wa ligi baada ya kushinda mechi mbili za ligi mfululizo, alisema kukosekana kwa kiungo huyo mshambuliaji kumeiathiri timu yake kimtindo hasa wakati huu ambao washambuliaji wake hawajaanza kufunga kwa kasi.

“Ni kweli Aziz Ki kukosekana kwake nafasi yake ilionekana lakini jambo zuri ni kwamba sasa amewasili na tutakuwa naye mazoezini leo (jana jioni) tunataka kumuangalia kama yuko sawasawa kwa kiasi gani,” alisema Gamondi.

“Alichelewa (Aziz) kutokana na kuuguliwa na mzazi wake lakini nadhani sasa tunatakiwa kuangalia mbele kwa kuwa tumeshakamilika kama familia kuelekea mchezo wetu ujao.

“Kurudi kwake (Aziz Ki) ni hatua moja, lakini kwanza tutaangalia yuko kwenye ubora wa namna gani ni muda kidogo tangu timu yake ilipotolewa kwenye Afcon.”

Yanga itakuwa ugenini kesho kuvaana na wenyeji wao Prisons katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Sokoine mkoani Mbeya.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA YANGA.....MBRAZILI SIMBA AINGIA KITETE NA 'MTETEMO' WA MAYELE...ONA ALICHOSEMA😂😂😂...