Home Azam FC SIKU CHACHE BAADA YA KUILIZA YANGA…MAYELE AMPONGEZA FEI TOTO KWA KAZI NZURI….

SIKU CHACHE BAADA YA KUILIZA YANGA…MAYELE AMPONGEZA FEI TOTO KWA KAZI NZURI….

FT:- AZAM FC 2-1 YANGA

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga SC, Fiston Mayele amempongeza kiungo wa Azam FC ambaye naye amewahi kukipiga Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ baada ya kufunga goli la ushindi wa 2-1 kwenye mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Feisal aliibuka Azam FC akitokea Yanga walipokutana kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi uliochezwa Machi 17, 2024 alipachika bao la ushindi dakika ya 52.

Mayele ambaye kwa sasa anaekipiga kwenye klabu ya Pyramid Misri, amempongeza Fei Toto kupitia kwenye post ambayo Feisal aliipost kwenye ukurasa wake inayoonyesha goli alilofunga kwenye mchezo huo na Mayele aliacha comment fupi “Hongera bro”.

Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Feisal kukutana na Yanga toka ajiunge na Azam FC na linakuwa goli lake la kwanza kuiwamba Yanga toka aondoke kwenye viunga vya twiga na Jangwani.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA MAMBO YA ZNZ...YANGA WATUMA SALAMU HII ALGERIA...