MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya DR Congo anayekipiga katika klabu ya Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele sasa ni kama anajipigia debe kutaka kusajiliwa na klabu ya Simba, akisema timu hiyo inatakiwa iwe na straika anaweza kuamua matokeo, huku akifunguka kuwa amefunguka na kusema lolote linawezekana juu ya kujiunga na Wekundu wa Msimbazi msimu ujao.
Kauli ya Mayele aliitoa jana mara baada ya kutembelea kambi ya Simba nchini Misri ambapo walikuwepo kucheza mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya nchini humo.
Mayele amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba kwa msimu ujao kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa imekuwa butu licha ya kuwepo kwa Fred Michael, Pa Omar Jobe ambao wamesajiliwa katika kipindi cha dirisha dogo.
Mayele amesema amefanikiwa kuitazama Simba katika mashindano ya kimataifa na kuona tatizo la safu ya ushambuliaji, ambayo ilikuwa na uwezo wa kuamua matokeo, kitu ambacho ni kama vile anajipigia debe kwa viongozi wa klabu hiyo ili kumtwaa msimu ujao kwa sababu yeye ndiyo mmoja wa mastraika wachache Afrika wenye uwezo huo.
Amesema katika mashindano makubwa safu ya ushambuliaji ndiyo wa kuamua matokeo kwa sababu michezo hiyo ni kutumia nafasi zinazopatikana ni vema kuzitumia vizuri.
โSiongei hayo kwa sababu mimi ni mshambuliaji, bali kwa kuwa nimeangalia mchezo wa Kimataifa. Kuhusu kujiunga na Simba ni suala tuombe Mungu nimalize msimu na lolote linawezekana,โ amesema Mayele.
Kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha yupo kwenye mtihani mgumu kwa sababu ya kutokuwa na washambuliaji wenye uwezo unaowapa nafasi ya kikosi cha kwanza katika mashindano ya kimataifa.
Majuma yaliyopita kocha huyo ameweka wazi kwamba wanahitaji kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi kubwa.