Home Habari za michezo KUHUSU UTATA WA GOLI LA AZIZI KI….CAF WAANZA UCHUNGUZI RASMI…ISHU NZIMA HII...

KUHUSU UTATA WA GOLI LA AZIZI KI….CAF WAANZA UCHUNGUZI RASMI…ISHU NZIMA HII HAPA…

Habari za Yanga

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limethibitisha rasmi kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu Mchezo wa robo fainali (CAF-CL), Mamelodi Sundowns dhidi ya Young Africans SC.

Imethibitishwa kuwa, majibu ya maombi hayo ya Wananchi wa Mitaa ya Twiga na Jangwani yatatoka muda wowote wiki hii kuanzia ijayo.

Taarifa zinaeleza kuwa, juzi Jumanne kamati ya mashindano ya (CAF) itafanya kikao, moja ya agenda ni mechi ya Mamelodi dhidi ya Yanga SC.

Itakumbukwa kuwa, Yanga waliandika barua kwa CAF wakitaka uchunguzi kuhusu tuhuma za upangaji matokeo baada ya kunyimwa bao alilofunga kiungo wao mshambuliaji Stephane Aziz Ki wakati wa mchezo wa marudiano wa robo fainali ya CAFCL, usiku wa Ijumaa iliyopita nchini Afrika Kusini.

Akithibitisha kupokelewa kwa barua hiyo, Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Qakili Patrick Simon amesema ni kweli wamepeleka malalamiko hayo na yamepokelewa CAF, na sasa uchunguzi unaendelea, hivyo taratibu zitakapokamilika watapewa majibu rasmi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMTAMBULISHA MBURUNDI WA NEWCASTEL JANA...MASHINE NYINGINE HII HAPA ITATUA YANGA...BANDO MUHIMU...