Home Habari za Yanga BOSI YANGA AWAGEUKIA MASHABIKI…”HUWEZI KUSEMA TUMESHINDA…VIONGOZI WA MATAWI KIKAANGONI

BOSI YANGA AWAGEUKIA MASHABIKI…”HUWEZI KUSEMA TUMESHINDA…VIONGOZI WA MATAWI KIKAANGONI

Habarii za Yanga leo

Mechi dhidi ya Simba Jumamosi ni fainali ya ubingwa wao kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo.

Amesisitiza kwamba kama kuna mtu anadhani uongozi wao
unaichukulia poa mechi hiyo basi anakosea kwani wao wanajua wanakwenda kucheza fainali itakayoamua nani anaufuata ubingwa msimu huu.

Gumbo alisema eneo la ufundi huko wamemuachia kocha wao ambapo wao viongozi watakutana na matawi ya Yanga kuhakikisha wanajipanga sawasawa kwa hesabu za umakini nje ya uwanja.

Aliongeza kuwa wanautaka ushindi wa mchezo huo ili kurahisisha na kubariki safari yao ya kuchukua ubingwa wa tatu mfululizo huku pia ushindi wa pili mbele ya watani wao hao.

Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo Yanga ikiwa mgeni ilishinda kwa mabao 5-1 ushindi ambao uliitibua Simba na kuamua kufukuza baadhi ya makocha wake kufuatia matokeo hayo.

“Huwezi kusema unashinda mechi kubwa kama hii bila kuonyesha kwa vitendo kwamba unataka ushindi, tumerudi sasa tunaingia na akili zote kwenye maandalizi ya mechi hii kubwa, hawa ni wakubwa wenzetu lazima tufanye maandalizi makubwa,” alisema Gumbo.

“Hatuna wasiwasi na kikosi chetu na masuala ya ufundi tumewaachia makocha wetu sisi kama viongozi kuna maeneo tutakwendakumalizia tu baada ya kukamilisha programu ya makocha.

“Huku nje tunataka kuhakikisha tunajipanga sawa sawa hatutaki kuona watu wanadhani tumeshashinda mechi hii, uzoefu unajieleza juu ya mambo uya namna hii tutakutana na uongozi mzima wa matawi kujadiliana haya yote haraka tunataka kuona kila mmoja anakuwa makini na huu mchezo.”

Wakati uongozi ukisema hayo kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema ingawa wanatambua ugumu na umuhimu wa matokeo ya mchezo huo lakini kambi yao itakayoanza leo itazingatia kwamba kikosi chake kinakwenda kuikabili Simba ngumu.

Gamondi alisema “Tunajua ugumu wa huo mchezo hapa hakuna tena matokeo ya kwamba tuliwafunga hii ni mechi mpya itakayokuwa na presha tofauti lakini kwetu sisi hatutaki kucheza kwa presha wala kuingia kwenye mchezo huo na presha.”

“Tunawaheshimu Simba ni timu kubwa ina makocha wazuri na wachezaji wazuri lakini kwetu sisi tunakwenda kutafuta ushindi kwa falsafa yetu, kuna mambo machache tunaweza kubadilisha hii ni mechi ya watani lazima tuwe makini lakini tutacheza kwa kufurahia mchezo tukitafuta ushindi.

“Hii ni mechi ambayo itazidi kutupa pointi tatu za kuukaribia ushindi hatutataka kufanya makosa yoyote yatakayotughalimu kwenye mipango yetu nawaamini wachezaji wangu,”alisisitiza.

SOMA NA HII  'UMC' WA VICHORONI WA MANARA WAMTIA MATATIZONI RAIS WA YANGA....TFF WAMFUNGULIA MSHITAKA HAYA...