Habari za Yanga
KIUNGO HUYU MSHAMBULIAJI YANGA HALI TETE…MCHAKATO WAANZA KUTIMKIA TIMU HII
Marce Ben Komba
April 30, 2024
9:24 pm
Bingwa wa Championship 2023-24 Kengold FC imeanza mchakato wa kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Yanga SC Farid Mussa kwa ajili ya kujiunga na wababe hao kutokea Jijini Mbeya.
Farid Mussa ambaye amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza ndani ya kikosi cha mkufunzi Miguel Gamondi amewekewa kandarasi ya miaka 2 mezani kwa ajili ya kuwatumikia Kengold kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-25.