Home Habari za michezo MAAMUZI MAGUMU SIMBA YAWE NI PAMOJA NA KUMPIGA CHINI INONGA…

MAAMUZI MAGUMU SIMBA YAWE NI PAMOJA NA KUMPIGA CHINI INONGA…

Habari za Simba

Katika yale maamuzi magumu ambayo viongozi Klabu ya Simba wanapaswa kuyafanya wakati huu bila kufikiria mara mbili mbili ni pamoja na kumuuza Henock Inonga.

Body language ya Inonga wa sasa hivi kwenye pitch si yule wa misimu miwili ya nyuma, huioni seriousness yake wala kujutia makosa yanayojirudia rudia. Kuna namna kama moyo wake haupo tena kuipambania Simba.

Inawezekana yupo kimwili, lakini sio kiakili, hata uchezaji wake hajitumia kama zamani, mara nyingi anaonekana anatembea na hata hakabi kwa nguvu ile aliyokuja nayo Simba.

Kwenye mitandao yake ya kijamii, Inonga ameweka emoji za kulia na kuaga huku akiandika ‘bye’ (kwa heri/kwa herini) bila kufafanua.

Kwa taswira hiyo hakuna room ya kumshawishi kubaki bali kumfungulia milango atafute changamoto mpya. Klabu itapoteza beki mkubwa, lakini itaingiza pesa ndefu ya kutafuta Inonga mwingine wa daraja la juu. Wapo wengi sokoni.

SOMA NA HII  WAKATI WAKIENDELEA KUSHINDA KILAINI MECHI ZAO....MAYELE 'AAMUA KUJILIPUA' YANGA....