Home Habari za michezo SHABIKI SIMBA:- HATUWEZI KUIFUNGA YANGA…TUNAKWENDA KUDHALILIKA…TUTAKULA KIPIGO KIZITO

SHABIKI SIMBA:- HATUWEZI KUIFUNGA YANGA…TUNAKWENDA KUDHALILIKA…TUTAKULA KIPIGO KIZITO

SHABIKI SIMBA:- HATUWEZI KUIFUNGA YANGA...TUNAKWENDA KUDHALILIKA...TUTAKULA KIPIGO KIZITO

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Mzee Mchachu amesema kuwa hatokwenda kwenye mchezo wa dabi dhidi ya watani zao Yanga Sc kwani anaamini kabisa timu yake ni mbovu na itakwenda kudhalilika kwa kipigo kizito siku hiyo.

Mchachu amesema hayo kueleka mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba utakaopigwa Jumamospi, Aprili 20, 2024 katika Dimba la Mkapa huku Simba wakiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao 5-1 na Yanga kwenye mchezo wa duru ya kwanza.

“Ligi tunaipoteza, sina Imani tena na Simba na hiyo mechi na mtani ninasema kabisa uwanjani siendi. Simba ikishinda basi ni rehema za Mwenyezi Mungu tu ila mimi siendi na sitaki.

“Najua kwa namna yoyote kama mtani anataka kikombe, hiyo mechi hatuachi, nasema Simba tukitoka droo basi tukachinje mbuzi, Yanga watatufunga.

“kama wachezaji wanacheza vile nalenale, mpira hautaki nalenale bana, mpira unataka kazi,” amesema mzee Mchachu.

SOMA NA HII  KISA 'UKATA'...AUSSEMS 'UCHEBE' AWAPIGA MKWARA MABOSI ZAKE KENYA...NI KAMA ALIVYOWACHANA SIMBA WAKATI ULE...