Home Habari za michezo WANANCHI WAJIPANGA KUPAMBANA NA WANAJESHI…WAINGIA KAMBINI LEO

WANANCHI WAJIPANGA KUPAMBANA NA WANAJESHI…WAINGIA KAMBINI LEO

HII SASA NOMA... YANGA YAMPANDISHA SANGOMA NDEGE...JEMEDARI SAID AFUNGUKA A-Z

Klabu ya Yanga imeingia kambini leo kwenye mazoezi baada ya kupata mapumziko ya siku moja kufuatia ushindi walioupata juzi Aprili 20, 2024 kwenye Dimba la Mkapa dhidi ya watani zao wa jadi, Simba SC.

Yanga ambao wanaongoza Ligi Kuu ya NBC mpaka sasa, kesho Aprili 23, 2024 watakuwa na kibarua kingine dhidi ya JKT Tanzania katika Dimba la Meja Jenerali Isamuyo, uliopo Bunju.

“Baada ya ushindi dhidi ya mtani (Simba SC), kikosi cha Wananchi Young Africans SC kimerejea mazoezini. Siku ya leo tunaelekea kujiandaa na mchezo unaofuata kesho dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo, Mbweni mkoani Dar es Salaam.

“Kikosi kimerejea mazoezini leo kutoa uchovu baada ya mapumziko siku ya jana na kila kitu kinakwenda sawa mpaka sasa. Wachezaji wameweza kufanya mazoezi viuri kujiandaa na mchezo wa kesho na kila kitu kinaenda vizuri.

“Wananchi ambao wapo dar es Slaam tunawahitaji sana kuja kutupa sapoti kama ambavyo imekuwa kawaida yenu, mmeweza kutupa sapoti mpaka hapa tulipofikia hatua chache kuelekea kwenye historia nyingine ambayo tunaenda kuiandika kwa pamoja. Jitokezeni kwa wingi kuja kutupa sapoti.

“Kila kitu kinaenda sawa mpaka sasa hivi, wachezaji wote wapo timamu kwa ajili ya mchezo isipokuwa Joyce Lomalisa ambaye alipata majeraha kidogo kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba, hatakuwa sehemu ya kikosi kesho lakini wachezaji wengine wapo sawa kabisa kukiwakilisha kikosi cha Wananchi siku ya kesho dhidi ya JKT Tanzania.

“Tunazihitaji alama tatu muhimu ambazo zitatusogeza kwenye ubingwa wetu wa 30. Njoo utusapoti tuandike pamoja historia, Wananchi tupo tayari kuendelea kuwapa burudani,” amesema Walter Harrison.

SOMA NA HII  BAADA YA KICHAPO CHA ZANACO...YANGA WAJIPOOZA LEO..WAICHAPA TIMU YA DARAJA LA KWANZA GOLI ZA KUTOSHA