Home Habari za michezo YANGA WAPIGA CHINI OFA YA AZAM YA MIL 400 KWA MZIZE….WAMSAINISHA MKATABA...

YANGA WAPIGA CHINI OFA YA AZAM YA MIL 400 KWA MZIZE….WAMSAINISHA MKATABA MPYA CHAP…

Habari za Michezo leo

UONGOZI wa Yanga umemuongeza mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao, Climate Mzize kuendelea kusalia ndani ya kikosi cha timu hiyo kwa misimu mingine ya mashundano ya ndani na kimataifa.

Hatua hiyo ni baada ya Azam FC Azam FC wametuma ofa ya 400 million kwa ajili ya kumuhitaji Mzize, ambapo ofa hiyo hakuna sehemu iliyoonyesha kubadilishana mchezaji kati ya nyota huyo ya Prince Dube ambaye yupo kwenye mgogoro na timu hiyo kwa sasa yupo sokoni.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga kuwa jana usiku viongozi walikutana na nyota huyo kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya na hatimaye mambo yakaenda sawa na kuongeza miwili.

“Mzize ameongeza mkataba tena ni mali ya Yanga, suala la ofa ya kwenda Azam FC sijui waje na ofa kubwa zaidi lakini kwa sasa hatuna mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo,” amesema chanzo hicho cha habari.

Kwa upande wa uongozi wa Azam FC umekiri kupeleka ofa na kuweka dau nono la kutaka huduma ya mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize kwa ajili ya msimu ujoa.

Mbali na ofa hiyo pia Azam FC wameonyesha nia ya kuhitaji saini ya kiungo wa Simba, Clatous Chama ambaye mkataba wake upo ukingoni na tayari mazungumzo na klabu yake yakiendelea kwa lengo la kumuongezea.

Ofisa habari Msaidizi wa Azam FC, Hashim Ibwe amebainisha wamepeleka ofa katika klabu mbili za Yanga na Simba kuhitaji baadhi ya nyota wanne ambao wamewaona katika klabu hizo.

Amesema Yanga wamepeleka maombi Yanga kumuhitaji Mzize kwa kuweka ofa nono mezani ikiwemo mshahara na mambo muhimu kwa ajili ya mchezaji huyo.

“Hatuishii kwa Yanga pekee pia wataenda na Simba na wiki ijayo kuanzia Jumatatu tunapeleka ofa nyingine kwenye moja ya hizi klabu tukihitaji huduma ya moja ya mchezaji wao,” amesema Ibwe.

Ameongeza kuwa msimu huu wamedhamilia kufanya usajili na kuchukuwa wachezaji wanne ndani ya klabu hizo mbili ikiwemo wachezaji wazawa na wakigeni.

Ibwe amesema wameamua kufanya kweli na hawataki masihara katika ofa hizo hakuna sehemu ambayo tunahitaji kubadilishana wachezaji bali wanaweka ofa mezani.

SOMA NA HII  KOCHA NABI, MORISSON WATUPWA NJE YA DIMBA FAR RABAT HAWANA CHAO