Home Habari za michezo AUCHO AWAGEUKIA WACHEZAJI…”MKITAKA NIWE MTU MBAYA NITAFANYA HIVYO

AUCHO AWAGEUKIA WACHEZAJI…”MKITAKA NIWE MTU MBAYA NITAFANYA HIVYO

Habari za Yanga leo

Kiungo mkabaji wa Klabu ya Yanga, Khalid Aucho ‘Daktari wa Mpira’ amesema kuwa iwapo watu wanataka awe mtu mbaya basi atafanya hivyo.

Aucho ambaye ametoka majeruhi aliyokaa kwa mwezi mzima ametoa kauli hiyo ikiwa ni mechi tatu mfululizo akifanyiwa, mmadhambi (fouls) za makusudi huku akiamini kuwa kisasi ni haki.

Mechi ya juzi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho la NBC dhidi ya Tabora, Aucho alishindwa kuendelea.
Jana Aucho aliandika maneno haya akimnukuu Zlatan Ibrahimovic; “Ikiwa unataka niwe mtu mzuri nitakuwa mtu mzuri na ikiwa unataka niwe mtu mbaya pia nitakuwa mtu mbaya,” amesema Aucho.

SOMA NA HII  TETESI:MZAMIRU KUONDOKA SIMBA...ATIMKIA TIMU HII BONGO...KIBU KUSAINI