Home Habari za michezo ENG HERSI NI MAFYA AISEE…KATUA CONGO KIMYA KIMYA KUMALIZANA NA MASHINE HII...

ENG HERSI NI MAFYA AISEE…KATUA CONGO KIMYA KIMYA KUMALIZANA NA MASHINE HII YA KAZI…

Habari za Yanga leo

RAIS wa Yanga, Hersi Said yupo nchini DR Congo na kufatilia baadhi ya wachezaji waliopendekezwa na Kocha Miguel Gamondi anawahitaji kuimarisha kikosi kwa ajili ya msimu ujao wa Mashindano.

Imeelezwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anawafatilia ni Chadrack Boka anayecheza nafasi ya “Left Back”, wa klabu ya Saint Eloi Lupopo inayoshiriki Ligi nchini humo.

Mtoa habari huyo amesema licha ya kufatilia mchezaji huyo lakini pia amekutana na Rais wa klabu ya TP Mazembe, Moesi Katumbi kwa lengo la kuzungumza na kujadilia mambo mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa timu lakini na suala zima la usajili wa wachezaji.

Taarifa za uhakika, kuwa Hersi yupo nchini humo kukamilisha dili la mchezaji (jina na nafasi hakuweka wazi) kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi chini ya Kocha Miguel Gamondi.

Amesema kocha huyo tayari ameshawasilisha ripoti ya awali kwa uongozi ambapo Rais huyo wa Yanga ameanza kufanyia kazi kwa kuangalia mchakato wa kufatilia wachezaji na nafasi zilizopendekezwa.

“Nafasi ya Mshambuliaji ndio imezingatiwa zaidi maana tangu alipoondoka Mayele (Fiston), hajapatikana mtu sahihi, walikuja bado hawajaweza kukidhi mahitaji ya safu hiyo lakini pia kuangalia nafasi zingine ikiwemo safu ya ulinzi kutaka kuimarisha eneo hilo ,” amesema mtoa habari huyo.

Yanga wapo katika mipango ya kuwaacha baadhi ya nyota wake akiwemo Joyce Lomalisa, Skudu Makudubela, Bakari Mwamnyeto ambaye hataongezewa mkataba na wakala wake kumtafutia timu Afrika Kusini.

Lakini pia kuna mvutano mkubwa upo kwa nani kati ya Augustine Okrah na Kennedy Musonda nani anatakiwa kuachwa huku wakipisha usajili wa mchezaji mwingine kwa ajili ya kuimarisha timu hiyo kwa msimu ujao.

Kwa mujibu wa Hersi Amesema mambo mazuri yanakuja ndani ya klabu hiyo kuhakikisha anaendelea kuwapa furaha mashabiki na wanachama wa Yanga.

Amesema mikakati yao ni kuendelea kuimarisha kikosi kwa kuongeza baadhi ya wachezaji ambao wamependekezwa na benchi la ufundi lakini kuwaongezea mikataba wale wote ambao imefikia ukingoni na wapo kwenye mipango ya timu.

SOMA NA HII  CHAMA: SIMBA WANAWEZA KUZIBA PENGO LANGU....