Home Habari za michezo JEMEDARI AWAVAA SIMBA NA YANGA…NI KUHUSU KUENDEKEZA USHIRIKINA…ISHU NZIMA HII HAPA

JEMEDARI AWAVAA SIMBA NA YANGA…NI KUHUSU KUENDEKEZA USHIRIKINA…ISHU NZIMA HII HAPA

JEMEDARI AWAVAA SIMBA NA YANGA...NI KUHUSU KUENDEKEZA USHIRIKINA...ISHU NZIMA HII HAPA

Jana (Juzi) Yanga SC wakiwa mazoezini Lake Tanganyika kuna watu walikuwa wanafanya vitendo vya kishirikina kabla ya mazoezi, Simba SC walifanya hivyo kabla ya Tabora United pale Tabora.

Adhabu ya Simba SC kutoka Bodi ya Ligi Kuu ilikuwa faini ya 1M tu. Lakini hivi vitendo ni vya hovyo sana na vinachafua hadhi ya Ligi Kuu kwa kiasi kikubwa sana. Bodi ya Ligi na TFF wanapaswa kulinda brand ya ligi kutokana na vitendo vya hovyo kama hivi na kuweka faini KUBWA.

Hizi timu ambazo zimecheza robo fainali ya CAF Champions League ndizi ambazo pia zinashindana kwenye mambo ya ULOZI pia. Zilipocheza zenyewe kwa zenyewe kwenye Ligi zimetozwa faini kwa kuamini mambo haya haya yasiyo na maana.

Timu hizi pamoja na kuongoza kwenye ubora wa mpira, zinaongoza pia kwenye mambo ya hovyo yanayodumaza mustakabali wa soka. Unahitaji watu wenye uthubutu kudhibiti upuuzi huu.
Tazama Video hapa chini;

SOMA NA HII  RAIS LA LIGA:- "ONYO BARCELONA HAMUWEZI KUNUNUA MCHEZAJI MNAYEMTAKA...MASTAA KUUZWA