Home Habari za michezo KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS…MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA

KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS…MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA

KELVIN JOHN KUIONGOZA TAIFA STARS...MSUVA,SAMATA,ZIMBWE JR WATEMWA

Mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Kelvin Pius John ‘Mbappe’ anatarajiwa kuongoza kikosi cha Taifa Stars kwenda nchini Saudi Arabia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan.

Ikiwa nchini humo Stars itacheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sudan kabla ya kurudi nchini kuendelea na ratiba zake nyingine.
Katika kikosi kilichoitwa na kocha Hemed Seleman ‘Morroco’ kuna namba kubwa ya wachezaji ambao ni makinda.

Kikosi kilichoitwa kina makipa Ahmed Ali Suleiman, Ally Salim na Abrahman Vuai Nassoro.

Mabeki ni Mukrim Issa Abdallah, Alphonce Mabula Msanga, Miano Danilo Van Den Bos, Gadiel Michael Kamagi, Abdulmalik Adam Zakaria, Baraka Shabaan Mtuwi, Abdulrahim Seif Bausi, Mohammed Ali Omar Sagaf.
Viungo ni Morice Michael Abraham, Khalid Habibud, Ishaka Said Mwinyi na Jabir Seif Mpanda

Washambuliaji ni Omary Abdallah Omary, Ben Anthony Starkie, Oscar Adam Paul, Tarryn Allarakhia na Ibrahim Hamad Ahmada na Kelvin.

SOMA NA HII  KISA KARIAKOO DABI YANGA YAPIGWA FAINI...KULIPA MAMILIONI HAYA...WAFANYA KOSA HILI