Habari za Simba leo
Habari za michezo

AHMED ALLY AWAPIGA DONGO HILI YANGA:- “MKIMNUNUA KIBU MTAFILISIKA

Marce Ben Komba May 11, 2024 9:54 am

Meneja wa Habari na Mawasiliano na Msemaji wa Klabu wa Simba SC, Ahmed Ally amesema mchezaji wao Kibu Denis ambaye alihusishwa kujiunga na watani wao wa jadi Yanga hatoondoka klabuni hapo na ikiwa watataka kumnunua wajiandae kufilisika na kwamba suala la malipo kwao sio shida.

Ahmed Ameyasema hayo katika mahojiano maalum na Crown media akifananisha suala hilo na kulitoa jua Mashariki lichomoze magharibi.

“Wana hatari ya kufilisika hao hawana uwezo wa kumiliki mchezaji aina ya Kibu, hawana cha kumlipa Kibu Denis Prosper hawana uwezo wa kuchukua mchezaji Simba Sports Club niamini mimi. Haiwezi kutokea yani ni sawa na kulitoa jua Mashariki lichomoze magharibi,” amesema Ahmed.

SIMBA KUMSAJILI MSHAMBULIAJI HUYU HATARI…TAYARI AMEOMBA KUONDOKA TIMU HIZI HATARINI KUSHUKA LIGI KUU…KMC, TZ PRISONS ZATAJWA…LIST KAMILI HII HAPA