Home Azam FC WAKATI YANGA WAKICHEKELEA KOONI….SIMBA, AZAM NI ‘MPERA MPERA MPAKA KIAMA’ πŸ˜‚πŸ˜‚….

WAKATI YANGA WAKICHEKELEA KOONI….SIMBA, AZAM NI ‘MPERA MPERA MPAKA KIAMA’ πŸ˜‚πŸ˜‚….

Habari za Simba leo

Simba inarudi katika uwanja wa nyumbani leo, itakapoikaribisha Geita Gold kwenye mchezo mgumu ambao kila timu itakuwa na hesabu zake, zikielekea kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara.

Hesabu za Simba ni kusaka pointi tatu zitakazoisadia kupata nafasi ya pili kwenye ligi inayowaniwa pia na Azam FC ambayo nayo itakuwa uwanjani dhidi ya JKT Tanzania ugenini.

Simba na Azam zote zina pointi 60 kwenye ligi lakini matajiri wa Chamazi wako nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, timu hizo zikiendelea kufukuzana kuwania nafasi ya pili itakayotoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Wakati Simba ikipambana kutafuta nafasi ya pili, Geita itakuwa uwanjani ikitaka ushindi ili kuepuka na dhahama ya kushuka daraja, ikiwa inashika nafasi ya 15 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 27 ikibakiza mechi tatu.

Rekodi zinaibeba Simba mbele ya Geita, Wekundu hao katika mechi tano walizokutana wameshinda nne na kutoa sare moja.

Simba inayofundishwa na Juma Mgunda imekuwa na mwendo mzuri tangu iwe chini ya kocha huyo mzawa ikiwa haijapoteza mchezo kati ya sita iliyocheza, ikiwa imeshinda minne na sare miwili.

Mshambuliaji Freddy Michael atakuwa na dakika 90 zingine zitakazompa nafasi ya kuendeleza moto wake wa mabao akiwa tayari ameshafunga sita yaliyorudisha kasi yake ya kufumania nyavu.

Kuelekea mechi hiyo itakayopigwa katika Uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:00 jioni, Mgunda amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi. β€œMaandalizi ya mchezo huu yamekamilika. Tunafahamu kwamba tunakwenda kucheza mechi ni ngumu dhidi ya Geita. Wanahesabu zao na sisi tuna zetu. Hii ni timu yenye wachezaji wazuri na kocha mzuri, kwa hiyo mashabiki wetu waje uwanjani kuwapa nguvu wachezaji wao,” alisema Mgunda.

Tangu Geita iwe chini ya kocha Denis Kitambi imecheza mechi 15 ikishinda mbili na kupoteza saba huku ikitoka sare sita ambapo imeendelea kuwa na matokeo yanayotia shaka.

Changamoto kubwa inayoitafuna ni ubutu wa safu ya ushambuliaji ambayo haijafunga bao lolote kwenye mechi tano zilizopita ambapo mara ya mwisho kupata bao ilikuwa Aprili 13,2024, ilipolazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Mtibwa Sugar.

β€œKubwa ni kwamba katika maisha yangu ya soka ni mara ya kwanza nakwenda kwenye mechi kubwa bila kuangalia ubora wa mpinzani na sijafanya hivyo kwa sababu soka ni mchezo wa wa magoli na sisi hatufungi. Kwa hiyo tumejikita kuwapa mbinu vijana ili waweze kutumia nafasi wanazotengeneza,” alisema Kitambi.

AZAM KAZI IPO

Baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), Azam FC leo itakuwa ugenini ikikaribishwa na JKT Tanzania kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Meja Isamuhyo.

Azam iko kwenye ushindani mkubwa na Simba ambao wanalingana pointi kwa sasa kwani katika mechi 27 walizocheza wawili hao, wote wana ya pointi 60 kila mmoja, wakitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufunga.

Azam inaanza wiki na maafande hao kwa hesabu za kutotaka kuruhusu mabao katika mechi hiyo ya 28 ili kuendelea kujiweka katika mikono salama ya kupata nafasi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Kwa Maafande hali si shwari kwani wako nafasi ya tisa wakiwa wamecheza mechi 27 sawa na wapinzani wao, na wataingia katika mechi hiyo wakiwa na kibarua cha kulinda nafasi.

JKT hawapo salama wakiwa na pointi 31 tofauti ya pointi tano tu na timu zinazoweza kushuka daraja.

SOMA NA HII  KUDADEKI..SIMBA HII NI MAFIA SANA AISEE...WATUMIA TRIKI ZA KIJASUSI KUIPOKONYA KIUNGO WYDAD CASABLANCA...