Home Habari za michezo GAMONDI:- KWA YANGA HII BADO HAIJAISHA MPAKA IISHE KABISA….

GAMONDI:- KWA YANGA HII BADO HAIJAISHA MPAKA IISHE KABISA….

Habari za Yanga leo

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kuwa na msimu mzuri bado wana kazi ngumu mbele yao katika fainali ya kombe la Shirikisho la CRBD Bank dhidi ya Azam FC.

Katika fainali hiyo Yanga atakuwa ugenini mbele ya wenyeji Azam FC, mchezo utakaochezwa Juni 2, mwaka huu uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar, saa 2:15, usiku.

Gamondi amesema anafurahi kufikia malengo yao kwa kutwaa taji la ubingwa wa ligi pamoja na mchezaji wake Stephane Aziz Ki kufanikiwa kumaliza msimu akiwa kinara wa ufungaji bora.

“Mwanzoni mwa msimu niliwaambia kuhusu Aziz Ki, kuwa ni mchezaji mkubwa na atafanya mambo makubwa anachukuwa tuzo ya mfungaji bora ni jambo la kujivunia. Licha ya yote lakini bado hatujamaliza kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni fainali,” amesema Gamondi.

Amesema wana fainali ya Shirikisho dhidi ya Azam FC, hautakuwa mchezo rahisi anaimani na vijana wake kufanya vizuri na kufanikiwa kutwaa taji hilo wakicheza vizuri na kufuata maelekezo yao.

“Msimu huu tumecheza vizuri, nimekuwa na timu bora, safu ya ulinzi, viungo na washambuliaji kisa kufanikiwa kuchukuwa tuzo ya ufungaji bora sasa tunaelekeza nguvu kwenye fainali yetu dhidi ya Azam FC.

Fainali ni timu mbili kati ya hizo lazima mmoja apate ushindi. Yanga kwangu ni timu bora kwa hapa nchini na tunaenda kucheza fainali kwenye uwanja mzuri ambao unachezeka vizuri,” alisema kocha huyo.

Gamondi ameeleza kuwa hautakuwa fainali rahisi kulingana na mechi ya mwisho walipokutana na Azam FC, walipoteza hali ambayo hataki kuona inajirudia katika fainali hiyo.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA MBINU ALIZOWAPA WACHEZAJI WA SIMBA