Home Habari za michezo HII HAPA ‘VITA’ YA KIMYA KIMYA KATI YA TSHABALALA NA YAO KOUASSI...

HII HAPA ‘VITA’ YA KIMYA KIMYA KATI YA TSHABALALA NA YAO KOUASSI ….MAMBO NI 🔥🔥🔥….

Habari za Michezo leo

MPIRA wa adhabu alioupiga na kusababisha bao la pili dhidi ya Azam FC, Alhamisi iliyopita kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, akiiwezesha timu yake ya Simba kushinda mabao 3-0, umemfanya beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, kufikisha idadi ya pasi za mabao sita mpaka sasa na kumsogelea kwa karibu kinara wa ‘asisti’ upande wa walinzi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yao Kouassi wa Yanga.

Kwa mujibu wa dawati letu la takwimu, Kouassi, raia wa Ivory Coast, anayecheza beki wa kulia, anaongoza kwa ‘asisst’ kwa mabeki, akiwa ametoa pasi saba mpaka sasa, lakini tayari ameanza kuwekwa kwenye hali ya hatari na Tshabalala ambaye, faulo yake iliyofungwa kwa kichwa na Fabrice Ngoma imemfanya kumsogolea kwa karibu.

Wakati kukiwa na vita ya kuwania kiatu cha dhahabu kati ya Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum, ‘Fei Toto’, tayari kumezuka nyingine ya ‘asisti’ upande wa mabeki, huku Ligi Kuu ikielekea ukingoni ambapo imeingia raundi ya 27.

Nafasi ya tatu inashikiliwa na mabeki wawili wa Azam FC, Pascal Msindo anayecheza beki wa kulia, Lusajo Mwaikenda na Rahim Shomari wa KMC wenye ‘asisti’ tano kila mmoja.

Nickson Kibabage wa Yanga na Shomari Kapombe wa Simba, ambao wote wanacheza beki wa kulia, wana ‘asisst’ nne mpaka sasa.

Wachezaji wanaoongoza kwa ‘asisti’ za jumla ni Kipre Junior wa Azam FC na Aziz Ki wa Yanga, ambao wote wana ‘asisst’ nane kila mmoja, wakifuatiwa na Fei Toto wa Azam na Kouassi wa Yanga, ambao wote wana ‘asisti’ saba kila mmoja.

SOMA NA HII  TONOMBE KUINGIA ANGA ZA HOROYA YANGA WAFUNGUKA