Home Habari za michezo KUHUSU AZIZI KI NA FEI TOTO KUTUA SIMBA MSIMU UJAO…AHMED ALLY AANIKA...

KUHUSU AZIZI KI NA FEI TOTO KUTUA SIMBA MSIMU UJAO…AHMED ALLY AANIKA UKWELI ULIVYO…

Habari za Michezo

Klabu ya Simba imesema ina mpango wa kufanya kufuru kwenye usajili wao msimu ujao ikiwa ni pamoja na kuwachukua nyota kadhaa wa Yanga na Azam Fc akiwemo Stephanie Aziz Ki na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwasili Dar es Salaam wakitokea Dodoma ambako Simba ilikuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji wiki iliyopita.

“Ni kweli hao wachezaji wawili wapo kwenye mipango yetu mmoja mkataba wake umefikia ukingoni na bado hajasaini mkataba mpya, kwa Fei Toto ni suala la kuweka fedha mezani ili kumchukua.”

“Pia kuna wachezaji wengine wapya tunawafuatilia sokoni kulingana na mapendekezo ya Benchi la Ufundi kwa ajili ya kuwasajili na kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao”

“Muda sio mrefu uongozi wa klabu utawasilisha ofa Azam FC kuangalia uwezekano wa kumsajili Fei Toto ambaye amekuwa sehemu ya vikosi vya timu za taifa Taifa Stars na Zanzibar Heroes,” amesema Ahmed Ally.

Aziz Ki na Fei Toto wote ni vinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ambapo mpaka sasa wana mago 15 kila mmoja lakini hata hivyo mikataba wa Aziz ndani ya Young Africans unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Mbali na Simba SC pia inaelezwa kuna timu kutoka Afrika Kusini ambazo zinafanya mchakato wa kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Burkina Faso.

SOMA NA HII  MINZIRO KAWATAZAMA YANGA WEEE..KISHA AKASHIKA KIDEVU NA KUSEMA HAYA...