Home Habari za michezo KUHUSU KUHUSISHWA SIMBA, YANGA…KELVIN JOHN AFUNGUKA NI WAPI ANAENDA….

KUHUSU KUHUSISHWA SIMBA, YANGA…KELVIN JOHN AFUNGUKA NI WAPI ANAENDA….

Habari za Michezo leo

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Kelvin John ‘Mbappe’ anayecheza soka la kulipwa katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji amesema mkataba alionao na klabu hiyo unamalizika Juni 30, mwaka huu, lakini hana mpango wa kurudi kucheza hapa nchini.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Genk, Julai Mosi, 2023 kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza miwili endapo atafanya vizuri.

Akizungumza na gazeti la  Mwanaspoti, Mbappe amesema ni kweli mkataba wake unaelekea mwishoni, lakini bado hajafikiria kurudi Tanzania kucheza Ligi Kuu Bara kiu yake ikiwa ni kuendelea kubaki huko akipambana kusaka maisha mengine.

“Mkataba wangu unaelekea ukingoni nimebakiza mwezi tu na mazungumzo na timu yangu yanaenda vizuri na kuhusu kurudi Tanzania hapana na hata nikipata ofa siwezi kuja huko, kwani ndoto yangu ni kusoka mbele na sio kurudi nyuma,” amesema nyota huyo anayeichezea timu ya taifa na kuongeza:

“Umri wangu unaniruhusu kuendeleza mapambano huku na nina imani kubwa ya kuendelea kubaki, kwani ofa zipo nje ya timu ninayoitumikia na timu zimeonyesha nia ya kuwa na mimi.”

Licha ya wadau wengi kumtaja kuwa mchezaji huyo kiwango chake kinashuka mwenywe ameweka wazi kuwa anafurahia maisha ndani ya timu hiyo na mipango yake inaenda vizuri ni suala la muda kuamua kutimka au kuendelea kubaki.

“Kushuka kiwango hili linatakiwa kuzungumzwa na kocha ambaye ananisimamia maneno ya wadau yapo siku zote huwa siyapi kipaumbele nazingatia kazi yangu ambayo inaniingizia kipato,” amesema mchezaji huyo.

SOMA NA HII  HIZI HAPA DK 90 ZA MWISHO KWA MBRAZILI SIMBA...AKISHINDWA HAPA TENA ULE UTABIRI UTATIMIA...